Vipengele Na Vidhibiti - Briggs & Stratton 2691184-00 Manual Del Operador

Tabla de contenido
Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 17
E
Ikoni za Lebo za Usalama
Linganisha kila ikoni ya lebo ya usalama hapa chini na jedwali
lifuatalo.
1
ONYO: Soma na uelewe Mwongozo wa Mwendeshaji kabla ya kutumia
mashine hii. Fahamu eneo na utendaji wa vidhibiti vyote. Usiendeshe
mashine hii ispokuwa ikiwa umepitia mafunzo.
2
HATARI - HATARI YA KUKOSA NGUVU YA KUKAMATA ARDHI,
KUTELEZA, KUENDESHA NA UDHIBITI KWENYE MTEREMKO:
Ikiwa mashine itasimama kwenda mbele au itaanza kuteleza kwenye
mteremko, simamisha visu na uendeshe polepole kutoka kwenye
mteremko.
3
HATARI: HATARI YA MOTO: Weka kifaa bila nyasi, majani na oili
nyingi kupita kiasi. Usiongeze mafuta wakati injini ipo moto au
inaguruma. Zima injini, ondoa ufunguo na uiruhusu ipoe kwa angalau
dakika 3 kabla ya kuongeza mafuta. Usiongeze mafuta ndani ya
nyumba, katika trela lililofunikwa, gereji au maeneo mingine
yaliyofungwa. Safisha mafuta yaliyomwagika. Usivute sigara ukiwa
unaendesha mashine hii.
4
HATARI - HATARI YA KUINAMA NA KUTELEZA: Kata nyasi kwenda
juu na chini ya miteremko, sio kutoka upande mmoja hadi mwingine.
Usiendeshe kwenye miteremko iliyoinama zaidi ya digrii 10. Epuka
kupiga kona ghafla na kwa kasi wakati ukiwa kwenye miteremko.
5
HATARI - HATARI YA KUKATWA VIUNGO VYA MWILI: Ili uepuke
majeraha kutokana na visu vinavyozunguka na sehemu zinazotembea,
weka vifaa vya usalama (vizuizi, ngao na swichi) tayari na viwe
vinafanya kazi.
6
Usikate nyasi wakati watoto au watu wengine wapo karibu. Usiwahi
kubeba watu, hasa watoto, hata kama visu vimezimwa. Usikate nyasi
ukirudi nyuma isipokuwa kama inahitajika. Tazama chini na nyuma –
kabla na wakati wa kurudi nyuma.
7
Rejelea maelezo ya kiufundi kabla ya kufanya ukarabati au udumishaji.
Wakati unaiacha mashine, zima injini, weka breki ya kuegesha kwenye
sehemu ya kufunga na uondoe ufunguo wa kuwasha.
8
Katia nyasi mbali na watu na watoto. Ondoa vitu ambavyo vinaweza
kurushwa na visu. Usikate nyasi bila chuti ya kutoa nyasi kuwekwa.
9
Usikate nyasi bila chuti ya kutoa nyasi au kikamata nyasi kuwekwa.
10
Ili uepuke majeraha ya visu vinavyozunguka, kaa mbali na ukingo wa
deki na ukatie nyasi mbali na watu wengine.

Vipengele na Vidhibiti

Linganisha herufi katika Kielelezo 2 na vipengele na vidhibiti
vinavyolingana na mashine yako iliyoorodeshwa katika jedwali
lililojumuishwa.
Alama za Udhibiti
A
B
C
D
E
F
Chaguo ya Kukata Nyasi Ukirudi Nyuma
(RMO)
Mita ya Saa (ikiwa ipo)
Swichi ya Kuwasha (Maeneo Tatu)
Zima
Endesha
Washa
Swichi ya PTO Juu (Washa)
Swichi ya Kiti ya PTO
Swichi ya PTO Chini (Zima)
61
Tabla de contenido
loading

Tabla de contenido