Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka
kwa haraka sana. Kuwa mwangalifu sana unapogusana na
mafuta. Kukosa Kuzingatia maagizo haya ya usalama
kunaweza kusababisha moto au mlipuko ambao unaweza
kupelekea majeraha mabaya ya kuchomeka au kifo.
• Zima injini na uwache injini ipoe kwa angalau dakika 3
kabla ya kuondoa kifuniko cha mafuta.
• Zima sigara, viko, na vyanzo vingine vyote vya mwako.
• Jaza tangi la mafuta nje au katika eneo lenye hewa nyingi
safi.
• Usijaze tangi la mafuta kupita kiasi. Ili uruhusu uvukizi wa
mafuta, usijaze hadi juu ya chini ya shingo la tangi la
mafuta.
• Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi,
joto, na vyanzo vingine vya mwako.
• Kagua tundu, tangi, kifuniko kama kuna nyufa na uvujaji.
Badilisha kama itahitajika.
• Mafuta yakimwagika, subiri mpaka pale ambapo
yatayeyuka kabla ya kuwasha injini na uepuke kuunda
chanzo chochote cha mwako.
• Tumia tu kontena za petroli zilizoidhinishwa.
1. Safisha kifuniko cha mafuta kutokana na uchafu na vifusi.
2. Ondoa kifuniko cha fueli (A, Kielelezo 5). Tazama sehemu
ya Vipengele na Vidhibiti.
3. Jaza tangi la mafuta (B) kwa mafuta. Ili uruhusu uvukizi wa
mafuta, usijaze hadi juu ya chini ya shingo la tangi la mafuta
(C).
4. Weka upya kifuniko cha Mafuta.
Washa injini.
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka
kwa haraka sana. Moto au mlipuko unaweza kusababisha
majeraha mabaya kuchomeka au kifo.
Wakati wa Kuwasha Injini
• Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha
mafuta, na kisafishaji hewa (iwapo kipo) vimefungwa na
kukazwa.
• Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
• Injini ikifurika, weka choki (ikiwa ipo) katika eneo la
kuonyesha FUNGUA / ENDESHA (OPEN / RUN),
songeza kidhibiti injini (ikiwa kipo) hadi eneo la
kuonyesha HARAKA (FAST) na ushtue hadi injini iwake.
1. Weka breki za kuegesha. Sukuma pedali ya breki kabisa,
vuta JUU kwenye kidhibiti cha breki kabisa, na uwachilie
pedali ya breki.
2. Zima Swichi ya PTO kwa kuisukuma CHINI.
3. Weka kidhibiti injini katika eneo linaloonyesha HARAKA
(FAST) ili kuweka CHOKI.
Injini iliyoshika joto haihitaji choki.
4. Ingiza ufunguo ndani ya swichi ya kuwasha na uuzungushe
hadi eneo linaloonyesha WASHA / ANZISHA (ON / START).
Injini ikikosa kuwaka baada ya kujaribu mara kadhaa,
tembelea BRIGGSandSTRATTON.COM au uwasiliane na
muuzaji aliyeidhinishwa.
5. Baada ya injini kuwaka, songeza kidhiti injini hadi kasi nusu.
Pasha injini joto kwa kuiendesha kwa angalau sekunde 30.
6. Weka kidhibiti injini katika eneo linaloonyesha HARAKA
(FAST).
Katika hali ya dharura, trekta / injini inaweza kusimamishwa
mara moja kwa kuzungusha switchi ya kuwasha hadi eneo
linaloonyesha ZIMA (STOP). Ili kuzima kawaida, rejelea
Kusimamisha Trekta na Injini .
Kusimamisha Trekta na Injini
1. Achilia pedali za kasi ya ardhini (tazama Vipengele na
Vidhibiti ) hadi kwenye eneo la linalonyesha GIA HURU
(NEUTRAL).
2. Ukiwa bado kwenye nyasi, zima swichi ya PTO, kisha
usubiri sehemu zote zinazosonga zisimame.
3. Songeza kidhibiti injini eneo la linaloonyesha POLEPOLE
(SLOW).
4. Zungusha ufunguo wa kuwasha ili KUZIMA.
5. Ondoa ufunguo na uuweke katika mahali salama mbali na
watoto.
6. Weka breki za kuegesha.
a. Ili kuweka breki ya kuegesha, sukuma pedali ya breki
kabisa, vuta JUU kwenye kidhibiti cha breki kabisa, na
uwachilie pedali ya breki. .
b. Ili kuondoa breki ya kuegesha, sukuma pedali ya breki
kabisa, sukuma CHINI kwenye kidhibiti cha breki kabisa,
na uwachilie pedali ya breki. .
Kukata Nyasi
Hatari
Mashine ina uwezo wa kukata mikono na miguu na kurusha
vitu. Kukosa kuzingatia maagizo ya usalama kunaweza
kusababisha kifo au majeraha mabaya.
• Endesha mashine tu wakati wa mchana au ukitumia taa
yenye mwangaza mzuri.
• Epuka mashimo, matope, matuta au hatari niyngine fiche.
Maeneo ambayo si tambarare yanaweza kufanya mashine
kubingirika au kumfanya mwendeshaju kupoteza mizani au
kuanguka.
• Usielekeze vitu vinavyotolewa kuelekea kwa mtu yeyote.
Epuka kuelekeza kwenye ukuta au kizuizi, vitu
vinavyotolewa kwni vinaweza kumrudia mwendeshaji.
• Simamisha visu unapovuka sehemu zenye changarawe.
65