mtembelee muuzaji wako. Ikiwa unahitaji kubadilisha betri, fuata
hatua za Kusafisha Betri na Kebo .
Ili kuchaji betri, fuata maagizo yaliyotolewa na mtengenezaji
kifaa cha kuchaji betri na vilevile onyo zote zilizojumuishwa
katika sehemu ya kanuni za usalama za kitabu hiki. Chaji betri
hadi ijae kabisa. Usichaji katika kiwango kikubwa zaidi kuliko
10 amps.
Kagua Muda wa Kusimama wa Visu vya
Mashine ya Kukatia Nyasi
Onyo
Visu vya mashine ya kukatia nyasi vikikosa kusimama kabisa
ndani ya sekunde 5, ni lazima klachi isongeshwe. Usiendeshe
mashine hiyo mpaka urekebishaji mwafaka uwe umefanywa
na muuzaji aliyeidhinishwa.
Visu vya kukatia nyasi na mkanda wa kuendeshea mashine ya
kukatia nyasi zinafaa kusimama kabisa ndani ya sekunde tano
baada ya swichi ya umeme ya PTO kuzimwa. Ikiwa mkanda
wa mashine ya kukatia nyasi hautasimama ndani ya sekunde
tano, mtembelee muuzaji aliyeidhinishwa kufanya ukarabati.
Badilisha Oili ya Injini na Chujio
1. Washa injini hadi ipate joto.
2. Weka trekta katika eneo tambarare.
3. Zima injini na uondoe ufunguo.
4. Safisha eneo la kujazia oili na chujio la oili kutokana na
vifusi vyovyote.
5. Ondoa kifaa cha kupima oili na ukiwekelee kwenye kitambaa
safi.
6. Tenganisha bomba laumwagaji oili (tazama Kielelezo 8).
7. Ondoa kifuniko kwa uangalifu na uteremshe bomba kwenye
kontena iliyoidhinishwa (C).
8. Baada ya oili kumwagwa, funika na ukazei, kisha
uunganishe bomba kwenye upande wa injini.
9. Ondoa chujio la oili (A, Kielelezo 9) na ulitupe kwa njia
inayofaa.
10. Lainisha kidogo kwenye gasketi ya chujio la oili ukitumia
oili safi.
11. Weka chujio la oili ukitumia mkono hadi gasketi igusane na
adapta ya chujio la oili, kisha ukaze chujio la oili kwa
mizunguko ya 1/2 hadi 3/4.
12. Ongeza oili (tazama Kagua na Uongeze Oili ya Injini ).
Kufunga Chujio la Hewa
Onyo
Usiwahi kuwasha au kuendesha injini huku kisafishaji hewa
au chujio la hewa zikiwa zimeondolewa kwani ni hatari ya
kusababisha moto.
68
Notisi
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio.
Hewa iliyoshinikizwa inaweza kuharibu chujio na maji
yatayeyusha chujio.
1. Legeza sehemu za kufunga (A, Kielelezo 10) na uondoe
kifuniko (B).
2. Fungua sehemu iliyofunga C) na uondoe chujio la hewa
(D).
3. Ondoa kisafishaji cha kwanza (Eikiwa kipo) kutoka kwenye
chujio la hewa.
4. Ili kulegeza vifusi, gongesha chujio la hewa kwa utaratibu
kwenye eneo gumu. Ikiwa chujio la hewa ni chafu kupita
kiasi, badilisha kwa chujio mpya.
5. Osha kisafishaji cha awali katika sabuni ya maji na maji.
Kisha kiwache kikauke kabisa kwenye hewa kavu. Usipake
oili kwenye kisafishaji cha awali.
6. Funga kisafisha cha awali kwenye chujio la hewa.
7. Weka kisafishaji hewa kwenye injini na ufunike.
8. Funika kifuniko na ukaze sehemu za kukazia.
Kagua Plagi za Spaki
Onyo
Cheche zinazotokea kwa bahati mbaya zinaweza kusababisha
moto au mrusho wa umeme.
Uwashaji usiotarajiwa unaweza kusababisha kunaswa,
kukatwa kwa viungo kwa kiwewe, au majeraha makali ya
ukataji wa ngozi.
Wakati wa kujaribu cheche:
• Tumia kifaa kilichoidhinishwa cha kujaribu plagi ya spaki.
• Usikague cheche huku plagi ya spaki ikiwa imeondolewa.
Notisi
Plagi za spaki zina ustahimilivu tofauti kwa joto. Ni muhimu
kwamba plagi sahihi ya spaki itumiwe, la sivyo, injini inaweza
kuharibika.
Safisha Plagi ya Spaki
Safisha ukitumia brashi ya waya na kisu kigumu. USITUMIE
kikwaruzo. .
Kagua Pengo la Plagi ya Spaki
Tumia kifaa kilichoidhinishwa cha kupima pengo la plagi ya
spaki (A, Kielelezo 11) ili kukagua pengo lililo kati ya elektrodi.
Wakati pengo hili liko sawa, kifaa cha kupima pengo kitajikokota
kidogo unapokivuta kupitia kwenye pengo.
Ikiwa inahitajika, tumia kifaa cha kupima pengo la plagi za spaki
ili kurekebisha pengo kwa kukunja kwa utaratibu elektrodi
zilizokunjwa bila kugusa katikati mwa elektrodi au kauri.
Weka Plagi ya Spaki