Briggs & Stratton 2691184-00 Manual Del Operador página 66

Tabla de contenido
Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 17
• USIWACHE mashine ikiwa peke yake. Kila wakati egesha
mahali tambarare, zima kiambatisho, weka breki ya
kuegesha, zima injini, na uondoe funguo.
1. Kalia kiti na urekebishe kiti ili uweze kufikia vidhibiti vyote
vizuri.
2. Tumia Swichi ya Urefu wa Kukata (tazama Vipengele na
Vidhibiti ) kuweka urefu wa kukata katika kiwango
unachotaka.
3. Weka kidhibiti injini katika eneo linaloonyesha HARAKA
(FAST).
4. Wacha swichi ya PTO ili kuwasha visu vya kukata nyasi.
5. Toa breki ya kuegesha, kisha uanze kukata nyasi.
6. Sukuma pedali ya kudhibiti kasi ya ardhini ili uende mbele.
Wachilia pedali ili usimame. Unavyosukuma pedali chini
zaidi ndivyo trekta itakwenda haraka zaidi.
7. Ukimaliza kukata nyasi, zima PTO.
8. Simamisha trekta kwa kuwachilia pedali za kudhibiti kasi
ya ardhini, uweke breki ya kuegesha, na uzime injini.
Onyo
Injini itazima ikiwa pedali ya kurudi nyuma ikisukumwa wakati
PTO imewashwa na Chaguo la Ukataji Nyasi Ukirudi Nyuma
halijawezeshwa. Mwendeshaji anafaa kila wakati kuzima PTO
kabla ya kuendesha kwenye barabara, vinjia, au eneo lolote
ambalo linaweza kutumiwa na magari mengine. Kupoteza
nguvu kwa ghafla kunaweza kusababisha hatari.
Chaguo la Kukata Nyasi Ukirudi Nyuma
(RMO)
Hatari
Kukata nyasi ukirudi nyuma kunaweza kuwa hatari kwa
waliosimama Kando. Ajali za kuhuzunisha zinaweza kutokea
ikiwa mwendeshaji hayuko makini kwa kuwepo kwa watoto.
Mara nyingi watoto huvutiwa na mashine hiyo na shughuli ya
ukataji nyasi. Usiwahi dhania kwamba watoto watasalia kukaa
pale ulipowaona mara ya mwisho.
• Weka watoto mbali na eneo linalokatwa nyasi na chini ya
uangalizi mkubwa wa mtu mzima anayewajibika.
• Usiwahi kubeba watu, hasa watoto, hata kama visu
vimezimwa. Watoto wanaweza kuanguka na kujeruhiwa
vibaya sana au kuhitilafiana na uendeshaji salama wa
kifaa. Watoto ambao wamewahi kubebwa na kifaa hapo
awali huenda wakatokea ghafla katika eneo linalokatwa
nyasi wakitaka kubebwa tena na wagongwe au
kusukumwa na mashine hiyo.
• Usikate nyasi ukirudi nyuma isipokuwa kama inahitajika.
Kila wakati tazama chini na nyuma kabla na wakati wa
kurudi nyuma.
• Mashine ikikata nyasi ikirudi nyuma bila kuwezesha
Chaguo la Kukata Nyasi Ukirudi Nyuma, mtembelee
muuzaji aliyeidhinishwa mara moja.
66
Kukata Nyasi Ukirudi Nyuma
Chaguo la Kukata Nyasi Ukirudi Nyuma (RMO) humruhusu
mwendeshaji kukata nyasi akirudi nyuma.
Ili kuliwezesha:
1. Washa swichi ya PTO.
2. Zungusha ufunguo wa Chaguo la Kukata Nyasi Ukirudi
Nyuma (RMO) (tazama Vipengele na Vidhibiti ) hadi
WASHA (ON).
3. Taa ya L.E.D. itawaka.
4. Sasa mwendeshaji anaweza kukata nyasi akirudi nyuma.
Kila wakati PTO imewashwa, RMO inahitaji kuwezeshwa
upya. Ufunguo unafaa kuondolewa ili kuzuia ufikiaji wa
RMO.
Udhibiti wa Uendeshaji
KUWEKA:
1. Sukuma pedali ya kasi ya ardhini ya kwenda mbele.
2. Vuta juu kwenye kidhibiti cha uendeshaji (tazama Vipengele
na Vidhibiti ) wakati kasi umefikia kasi unayotaka. Kidhibiti
cha uendeshaji kitafunga katika moja ya sehemu zake tano
za kufunga.
KUTOA:
1. Sukuma pedali ya breki.
AU
2. Sukuma pedali ya kasi ya ardhini ya kwenda mbele.
Udumishaji
Chati ya Udumishaji
TREKTA NA MASHINE YA KUKATIA NYASI
Kila Baada ya Saa 8 au Kila Siku
Kagua mfumo wa kiusalama wa intaloki
Safisha vifusi kwenye trekta na deki ya mashine ya kukatia nyasi
Safisha vifusi kwenye chumba cha injini
Kila Baada ya Saa 25 au Kila Mwaka*
Tabla de contenido
loading

Tabla de contenido