sw
Kiswahili
Huduma ya Udhibiti wa Mafukizo
Ili kupata huduma ya udumishaji, ubadilishaji, au ukarabati wa vifaa na
mifumo ya kudhibiti mafukizo, wasiliana na kituo chochote kinachohitimu
cha kukarabati injini au mtoa huduma aliyehitimu wa kukarabati injini.
Hata hivyo, ili kupata huduma ya kudhibiti mafukizo ya "bila malipo", ni lazima kazi
ifanywe na muuzaji aliyeidhinishwa na kiwanda. Rejelea Kauli za Udhibiti Mafukizo.
Kabureta na Kasi ya Injini
Usifanye marekebisho kwenye kabureta au kasi ya injini. Kabureta ilifungwa
kiwandani ili kufanya kazi kwa ufanisi katika mazingira mengi. Usihitilafiane
na springi ya kidhibiti, viunganishaji, au sehemu nyingine ili kubadilisha kasi
ya injini. Iwapo marekebisho yoyote yanahitajika, wasiliana na Mtoa Huduma
Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kufanyiwa huduma.
ILANI: Mtengenezaji wa kifaa hubainisha kasi ya juu zaidi ya injini kama
ilivyosakinishwa kwenye kifaa. Usizidishe kasi hii. Iwapo huna uhakika kasi ya juu
zaidi ya kifaa hiki ni ipi, au kasi ya injini iilivyopangwa tangu kiwandani, wasiliana
na Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kupata usaidizi. Kwa
oparesheni salama na sahihi ya kifaa hiki, kasi ya injini inapaswa tu kurekebishwa
na mtaalamu wa huduma aliyehitimu.
Kutatua Matatizo
Ili kupata usaidizi, wasiliana na muuzaji wa karibu au nenda kwenye
BRIGGSandSTRATTON.COM au piga simu kwa nambari 1-800-444-7774 (nchini
Marekani).
Kipimo kamili cha umeme kwa miundo ya injini za petroli kimewekwa kulingana
na SAE (Jamii ya Wahandisi wa Magari) msimbo J1940 Utaratibu wa Kipimo
cha Umeme & Mkufu wa Injini Ndogo na umepimwa kulingana na SAEJ1995.
Viwango vya mkufu vinafikia 2600 RPM kwa injini zenye "rpm" iliyowekwa
kwenye lebo na 3060 RPM kwa injini zingine zote; viwango vya nguvu ya injini
vinafikia 3600 RPM. Vizingo vya umeme kamili vinaweza kutazamwa katika
www.BRIGGSandSTRATTON.COM. Viwango jumla vya umeme vinachukuliwa
ekzosi na kisafishaji hewa zikiwa zimewekwa ilhali viwango vya umeme jumla
vinachukuliwa bila vipengee hivi kuwekwa. Nguvu kamili halisi ya injini itakuwa
juu zaidi kuliko nishati ya injini na yanaathiriwa na, miongoni mwa mambo
mengine, hali iliyoko ya kuendesha na utofauti wa injini hadi nyingine. Kukiwa
na bidhaa nyingi ambazo zimewekwa injini, injini ya petroli huenda ikakosa
kufikia kadirio la nguvu kamili inapotumiwa katika kifaa cha umeme. Tofauti hii
inatokana na vipengele mbalimbali zikijumuisha, lakini sio tu, vijenzi mbalimbali
vya injini (kisafishaji cha hewa, ekzosi, kuchaji, upunguzaji halijoto, kabureta,
pampu ya mafuta, n.k), vipimo vya matumizi, hali zilizoko za kuendesha (halijoto,
unyevunyevu, mwinuko), na utofauti kati ya injini moja hadi injini nyingine.
Kutokana na vipimo vya utengenezaji na uwezo, Briggs & Stratton wanaweza
kuibadilisha injini hii kwa injini iliyo na nguvu nyingi zaidi.
Udhamini
Waranti ya Injini ya Briggs & Stratton
Kuanzia Agosti 2022
Hakikisho lenye Kipimo
Briggs & Stratton inatoa waranti kwamba, wakati wa kipindi cha waranti
kilichobainishwa hapa chini, itafanyia ukarabati au kubadilisha, bila malipo,
kwa kutumia sehemu mpya au iliyotengenezwa upya, kwa uamuzi wa Briggs
& Stratton peekee, sehemu yoyote ambayo ina matatizo katika nyenzo au
ufanyakazi au yote mawili. Gharama za usafirishaji bidhaa zilizowasilishwa ili
kufanyiwa ukarabati au kubadilishwa chini ya hakikisho hili ni lazima zigharimiwe
na mnunuzi. Hakikisho hili linatumika na liko chini ya vipindi vya muda na masharti
yaliyoelezwa hapa chini. Ili kupata huduma ya waranti, tafuta Muuzaji Huduma
Aliyeidhinishwa aliye karibu zaidi nawe kwenye ramani yetu ya kutafuta wauzaji
kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM. Ni lazima mnunuzi awasiliane na Muuzaji
Huduma Aliyeidhinishwa, na kisha apeleke bidhaa kwa Muuzaji Huduma huyo
Aliyeidhinishwa ili kufanyiwa ukaguzi na majaribio.
Hakuna hakikisho lingine la haraka. Waranti zilizoashiriwa, ikiwa ni
pamoja na zile za uuzaji na uzima kwa ajili ya dhumuni fulani, zina
kipimo cha kipindi cha mwaka mmoja tangu kununuliwa, au kwa
kiwango kilichoruhusiwa na sheria. Waranti nyingine zote zilizoashiriwa
hazijumuishwi. Dhima ya uharibifu wa kimatukio au unaotokana na jambo
jingine haijajumuishwa kwa kiasi kinaruhusiwa na sheria. Baadhi ya majimbo
au nchi haziruhusu vipindi vya hakikisho kuwekewa vipimo, na baadhi ya majimbo
au nchi haziruhusu kutojumuishwa au kipimo cha uharibifu wa kimatukio au
unaotokana na jambo jingine, kwa hivyo kipimo na kutojumuishwa huku huenda
hakukuhusu wewe. Waranti hii hupeana haki maalum za kisheria na pia unaweza
kuwa na haki nyingine ambazo zinatofautiana kulingana na jimbo na nchi*.
Masharti Wastani ya Waranti¹, ²
Vanguard
; Msururu wa Kibiashara
®
Matumizi ya Kibinafsi - Miezi 36
Matumizi ya Kibiashara - Miezi 36
Msururu wa XR
Matumizi ya Kibinafsi - Miezi 24
Matumizi ya Kibiashara - Miezi 24
Injini Nyingine Zote Zenye Mkono wa Kalibu ya Chuma ya Dura-Bore™
Matumizi ya Kibinafsi - Miezi 24
Matumizi ya Kibiashara - Miezi 12
Injini Nyingine Zote
Matumizi ya Kibinafsi - Miezi 24
Matumizi ya Kibiashara - Miezi 3
¹Haya ni masharti yetu wastani ya waranti, lakini mara kwa mara huenda kukawa na
vipengele vya ziada vinavyosimamiwa na waranti ambavyo havikusimamiwa wakati
wa uchapishaji. Ili kupata orodha ya masharti ya sasa ya waranti ya injini yako,
nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM au uwasiliane na Muuzaji Huduma
wako Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton.
²Hakuna waranti kwa injini za vifaa vilivyotumiwa kutoa nishati badala ya kifaa
kinachofaa; jenereta ya akiba kwa madhumuni ya kibiashara, magari ya kubebea
mizigo yanayozidi 25 MPH, au injini zinazotumiwa katika mashindano ya mbio au
kwenye viwanja vya kibiashara au vya kukodishwa.
*Nchini Australia - Bidhaa zetu huja na waranti ambazo haziwezi kutojumuishwa
chini ya Sheria ya Mtumiaji ya Australia. Una haki ya kubadilishiwa au kurudishiwa
pesa kwa hitilafu kuu au fidia kwa uharibifu au hasara nyingine yoyote ya siku
za usoni. Pia una haki ya bidhaa kufanyiwa ukarabati au kubadilishwa endapo
bidhaa hazitakuwa za ubora unaokubaliwa na hitilafu haimaanishi kuharibika kwa
njia kubwa. Ili kupata huduma ya waranti, tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa
aliye karibu zaidi nawe kwenye ramani yetu ya kutafuta wauzaji kwenye
BRIGGSandSTRATTON.COM, au kwa kupiga simu kwa nambari 1300 274 447, au
barua kwa Briggs & Stratton Australia Pty Ltd, 1 Moorebank Avenue, Moorebank,
NSW, Australia, 2170.
Kipindi cha waranti huanzia tarehe ya ununuzi ya mtumiaji wa kwanza kununua
dukani rejareja au mtumiaji wa mwisho wa kibiashara, na inaendelea kwa kipindi
cha muda kilichobainishwa katika jedwali lililo hapa juu. "Matumizi ya kibinafsi"
inamaanisha matumizi ya kibinafsi ya nyumbani ya mtumiaji wa rejareja. "Matumizi
ya kibiashara" inamaanisha matumizi mengine yote, yakijumuisha matumizi kwa
madhumuni ya kibiashara, ya kuzalisha mapato au ya kukodisha. Pindi tu injini
inapopitia matumizi ya kibiashara, baada ya hapo itazingatiwa kuwa injini ya
matumizi ya kibiashara kwa ajili ya hakikisho hili.
Usajili wa bidhaa hauhitajiki ili kupata huduma ya waranti ya bidhaa za
Briggs & Stratton. Hifadhi risiti yako ya ushahidi wa ununuzi. Ukikosa
kutoa ushahidi wa tarehe ya kwanza ya ununuzi wakati huduma ya waranti
inapoombwa, tarehe ya utengenezaji wa bidhaa itatumiwa kubaini kipindi
cha waranti.
Kuhusu Hakikisho Lako
Hakikisho hili lenye kipimo linasimamia tu nyenzo zinazohusiana na injini na/au
utendakazi, na sio kubadilishiwa au kurudishiwa pesa ulizonunua kifaa ambacho
kina injini husika. Udumishaji, uimarishaji, marekebisho ya mara kwa mara au
®
kuchakaa na kuchanika kwa kawaida hazijasimamiwa na hakikisho hili. Vile vile,
hakikisho halitumiki ikiwa injini imehitilafiwa au kubadilishwa au ikiwa nambari
tambulishi ya injini imeharibiwa ua kuondolewa. Hakikisho hili halisimamii uharibifu
kwenye injini au matatizo ya utendakazi wa injini yanayosababishwa na:
1. Matumizi ya sehemu ambazo siBriggs & Stratton
2. Kuendesha injini zilizo na oili isiyotosha, chafu, au ya ubora usio sahihi;
3. Matumizi ya mafuta machafu au yaliyoharibika, petroli yaliyotengenezwa kwa
zaidi ya 10% ya ethanoli, au matumizi ya mafuta kama vile petroli iliyoevuka
au gesi asili kwenye injini ambazo hazijaundwa/kutengenezwa tangu mwanzo
na Briggs & Stratton kuendeshwa kwa mafuta kama hayo;
4. Uchafu ulioingia kwenye injini kwa sababu ya udumishaji kwa kutumia kisafishaji
hewa kisichofaa au ufunganishaji mbaya;
5. Kugonga kitu kwa visu vya kukata vya mashine ya kukatia nyasi, adapta, impela
au vifaa vingine vya shafti kombo ambavyo vimelegea au havijawekwa ifaavyo
au ukazaji wa v-belt kupita kiasi;
6. Sehemu au vifaa vinavyohusiana kama vile klachi, gia, vidhibiti vya kifaa, nk.,
ambavyo havijatolewa na Briggs & Stratton;
7. Joto kupita kiasi kutokana na vipande vya nyasi, uchafu na vifusi, au viota
vya panya vinavyoziba au kufunika vifaa vya kupoesha au eneo la gurudumu la
kuongeza kasi, au kuendesha injini bila uingizaji hewa wa kutosha;
8. Mtetemo kupita kiasi kwa ajili ya kasi kupita kiasi, uwekaji injini ikilegea, visua
kukata au impele ambazo zimelegea au havijasawazishwa, au uunganishaji
vibaya wa vipengele vya vifaa kwenye shafti kombo;
9. Matumizi mabaya, ukosefu wa udumishaji wa mara kwa mara, usafirishaji,
ushughulikiaji, au uwekaji injini vibaya.
Huduma ya hakikisho inapatikana tu kupitia Wauzaji Huduma Walioidhinishwa wa
Briggs & Stratton. Tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa aliye karibu zaidi nawe
kwenye ramani yetu ya kutafuta wauzaji kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM au
kwa kupiga simu kwa nambari 1-800-444-7774 (nchini Marekani).
80004537 (Rekebisho A)
29