Briggs & Stratton BPW4000 Manual Del Usuario página 201

Tabla de contenido
Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 60
Uhifadhi
Kama upangilii kutumia kioshaji kwa presha kwa zaidi ya siku 30,
lazima utayarishe injini na pampu kwa kuhifadhiwa.
Kuilinda Pampu
Ili kuilinda pampu dhidi ya uharibifu unaosababishwa na mabaki
ya madini au kuganda, tumia PumpSaver ili kuzuia uharibifu wa
kuganda na kulainisha pistoni na vinatishi.
ARIFA Kushindwa kulinda kitengo hiki dhidi ya halijoto ya
kuganda kutaweza kuharibu pampu na kufanya kitengo hiki
kutoweza kufanya kazi. Uharibifu wa kuganda haujajumulishwa
kwenye udhamini.
Kulinda Mfumo wa Mafuta
Mafuta yanaweza kuharibika endapo yatahifadhiwa zaidi ya siku
30. Mafuta yaliyoharibika yanaweza kusababisha mabaki ya asidi
na gamu na kufanya mabaki haya kubakia kwenye mfumo wa
mafuta au kwenye sehemu muhimu za kabyureta.
Hakuna haja ya kuondoa mafuta kutoka kwenye injini kama
kidhibiti cha mafuta kitaongezwa kulingana na maelekezo
yaliyotolewa. Endesha injini kwa dakika 2 ili kuzungusha kidhibiti
kwenye mfumo wote wa mafuta kabla ya uhifadhi.
Kama mafuta kwenye injini hayajatiwa dawa kwa kutumia kidhiti
cha mafuta, lazima yaondolewe na kuwekwa kwenye mkebe
ulioidhinishwa. Endesha injini mpaka pale itakaposita kutokana
na ukosefu wa mafuta. Matumizi ya kidhibiti cha mafuta kwenye
mkebe wa kuhifadhi yanapendekezwa ili kuhakikisha mafuta hayo
ni mazuri.
Vidokezo Vingine vya Uhifadhi
1. USIHIFADHI mafuta kutoka kwenye msimu mmoja hadi
mwingine isipokuwa tu kama yametiwa dawa kama
ilivyofafanuliwa katika Linda Mfumo wa Mafuta.
2. Funika kitengo hiki kwa kifuniko kinachofaa cha ulinzi
ambacho hakibakishi unyevunyevu.
ONYO! Fifuniko vya uhifadhi vinaweza kusababisha moto
na hatimaye kifo au majeraha mabaya. USIWEKE kifuniko
cha uhifadhi juu ya kioshaji kwa presha chenye joto.
Hakikisha kwamba mitambo hii imepoa kwa muda unaotosha
kabla ya kuweka kifuniko kwenye mitambo hii.
3. Hifadhi kitengo hicho katika eneo safi, kavu.
9 9
Tabla de contenido
loading

Tabla de contenido