Hudumia Plagi ya Spaki Kielelezo 3
Kubadilisha plagi ya spaki kutaiwezesha injini yako kuwasha
kwa urahisi na kunguruma vyema zaidi.
1. Legeza skrubu tatu za kifuniko cha udumishaji na uondoe
kifuniko chakando cha udumishaji (3).
2. Safisha sehemu iliyo na plagi ya spaki na uondoe kifuko
cha plagi ya spaki (9).
3. Ondoa plagi ya spaki na uikague.
4. Badilisha spaki ya plagi ikiwa elektrodi zimegubikwa,
zimeungua au kaulo imevunjika. Tumia plagi ya spaki
inayopendekezwa pekee. Tazama Maelezo.
5. Kagua pengo la elektrodi ukitumia geji (10) na usawazishe
pengo la plagi ya spaki hadi kiwango kilichopendekezwa
cha pengo ikiwa inahitajika (tazama Mapendekezo).
6. Weka plagi ya spaki na ukaze kabisa. Rejesha kifuko cha
plagi ya spaki.
7. Rejesha kifuniko cha kando cha udumishaji na ukitumia
mkno ukaze skrubu tatu za kifuniko cha udumishaji.
Kagua Kishika Cheche
Kagua kishika cheche kama kuna uharibifu au mzibo wa
kaboni. Iwapo kuna uharibifu au usafishaji unahitajika,
mtembelee Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs &
Stratton.
ONYO! Kugusana na eneo hili la mafla kunaweza
kusababisha kuchomeka na hivyo basi kupelekea
majeraha mabaya.
• Kuwa makini na maonyo yaliyo kwenye jenereta.
• Usiguse sehemu moto.
Uhifadhi
9 10
Ikiwa unahifadhi kifaa hiki kwa zaidi ya siku 30, tumia miongozo
ifuatayo ili kukiandaa kwa uhifadhi.
Linda Mfumo wa Mafuta
Mafuta yanaweza kuharibika ikihifadhiwa kwa zaidi ya siku 30.
Mafuta yaliyoharibika yanaweza kusababisha mabaki ya asidi
na gundi kutengenezeka kwenye mfumo wa mafuta au kwenye
sehemu muhimu za kabureta.
Hakuna haja ya kumwaga petroli kutoka kwenye injini ikiwa
kiimarishaji mafuta kimeongezwa kulingana na maagizo.
Washa injini ikiwa nje kwa dakika 2 kuzungusha kiimarishaji
katika mfumo wote wa mafuta kabla ya kukiweka.
Ikiwa petroli ndani ya injini haijatibiwa kwa kiimarishaji mafuta,
ni lazima imwagwe kwenye kontena iliyoidhinishwa. Kisha
endesha injini ikiwa nje hadi isimame kutokana na ukosefu wa
mafuta. Matumizi ya kiimarishaji mafuta kwenye kontena ya
uhifadhi yanapendekezwa ili kudumisha usafi.
kifo au majeraha mabaya.
• Unapohifadhi mafuta au kifaa chenye mafuta kwenye tangi,
hifadhi mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji, vifaa
vya kukausha nguo au vitu vingine ambavyo vina taa za moto
au vyanzo vya mwako kwa sababu vinaweza kuwasha moto
kwenye mivuke ya mafuta.
• Unapomwaga mafuta, zima injini na uwache injini ipoe kwa
angalau dakika 2 kabla ya kuondoa kifuniko cha mafuta.
• Legeza kifuniko hicho polepole ili kutoa shinikizo kwenye
tangi.
• Mwanga mafuta ukiwa nje ya nyumba.
• Weka mafuta mbali na cheche, moto ulio wazi, taa za gesi,
joto, na vyanzo vingine vya mwako.
• Kagua mifereji ya mafuta, tangi, kifuniko, na vijenzi mara kwa
mara kama kuna nyufa au uvujaji. Badilisha kama itahitajika.
Badilisha Oili ya Injini
Wakati injini ingali na joto, mwaga mafuta utoka kwenye
kifuniko cha kasha la shafti kombo. Jaza ukitumia ya ubora
unaopendekezwa. Tazama Kubadilisha Oili ya Injini.
Vidokezo Vingine vya Uhifadhi
1. USIHIFADHI mafuta kutoka kwenye msimu mmoja hadi
2. Hifadhi jenereta katika mahali safi na pakavu na uifunike
• Usiweke kifuniko cha uhifadhi juu ya jenereta iliyo moto.
• Wacha vifaa vipoe kwa muda wa kutosha kabla ya kuweka
kifuniko juu yake.
ONYO! Mafuta na mivuke yake yanaweza
kuwaka moto na kulipuka na kusababisha
kuchomeka, moto au mlipuko na kupelekea
mwingine isipokuwa tu kama yametiwa dawa kama
ilivyofafanuliwa katika Linda Mfumo wa Mafuta.
ukitumia kinga mwafaka ambayo haitasitiri unyevunyevu.
ONYO! Vifuniko vya uhifadhi vinaweza kusababisha
moto na hatimaye kifo au majeraha mabaya.
9