Briggs & Stratton Q6500 Manual De Instrucciones página 200

Ocultar thumbs Ver también para Q6500:
Tabla de contenido
Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 60
Hatua ya 5: Kuzima Jenereta
1. Zima na uondoe vifaa vyote vinavyotumia umeme kutoka
kwenye plagi za paneli ya jenereta. Usiwahi zima injini
huku vifaa vinavyotumia umeme vikiwa havijaondolewa na
vimewaka.
2. Acha injini iendelee kunguruma bila vifaa vinavyotumia
umeme kwa dakika moja ili kuimarisha hali joto la ndani ya
injini na jenereta.
3. Zungusha swichi ya injini hadi eneo linaloonyesha ZIMA
(OFF) (0).
Udumishaji
Ratiba ya Udumishaji
Fuata mpishano wa saa au kalenda, yoyote ile inayotangulia.
Huduma ya mara kwa mara zaidi inahitajika wakati
unapoendesha kwenye hali mbaya zaidi.
Saa 5 za Kwanza
Badilisha oili ya injini
Kila Baada ya Saa 8 au Kila Siku
Safisha vifusi
Kagua kiwango cha oili ya injini
Kila Baada ya Saa 25 au Kila Mwaka
Safisha chujio la hewa la injini
Kila Baada ya Saa 50 au Kila Mwaka
Kagua mafla na kishika cheche
Kila Baada ya Saa 100 au Kila Mwaka
Badilisha oili ya injini
Kila Mwaka
Badilisha chujio la hewa la injini
Badilisha plagi ya spaki
Fanya huduma mara nyingi zaidi katika hali chafu au zenye
1
vumbi.
Tembelea muuzaji huduma aliyeidhinishwa.
2
Mapendekezo Jumla
Udumishaji wa mara kwa mara utaboresha utendakazi na
kuongezea maisha ya jenereta ya nje. Tembelea Muuzaji
Huduma yeyote Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili
kuhudumiwa. Uwekaji sehemu na kazi kubwa ya ukarabati ni
lazima zifanywe na wafanyikazi wenye mafunzo maalum.
Hakikisho la jenereta halisimamii vifaa vilivyotumiwa vibaya
na kutelekezwa na mwendeshaji. Ili kupokea thamani kamili
ya hakikisho, ni lazima mwendeshaji adumishe jenereta jinsi
alivyoelekezwa kwenye mwongozo huu.
ONYO! Ili kuhakikisha usalama wa mashine, tumia tu
vipuri vya asili kutoka kwa mtengenezaji au
vilivyoidhinishwa na mtengenezaji. Ukiwa na maswali
kuhusu kubadilisha vijenzi kwenye jenereta yako, tafadhali
tutembelee kwenye tovuti yetu BRIGGSandSTRATTON.COM.
TAHADHARI Kasi za juu au chini zaidi kupita kasi
zinaweza kusababisha majeraha madogo. Usichokore
springi ya gavana, viungo au sehemu nyingine ili
kubadilisha kasi. Usifanye mabadiliko kwenye jenereta kwa njia
yoyote ile.
8
1,2
1
1
1,2
EU Stage V: Viwango vya CO2
Viwango vya CO2 vya injini zilizoidhinishwa za aina ya Briggs &
Stratton vinaweza kupatikana kwenue BriggsandStratton.com
kwa kucharaza CO2 ndani ya upau wa kutafuta.
Udumishaji Injini
Kubadilisha Oili ya Injini Mchoro Kielelezo 3 4 5 8
TAHADHARI Epuka oili ya mota iliyotumika
kugusana na ngozi kwa muda mrefu au mara nyingi.
Oili ya mota iliyotumika imeonekana kusababisha
saratani ya ngozi katika maabara fulani za wanyama. Safisha
kwa kina maeneo yaliyoathirika ukitumia sabuni na maji.
WEKA MBALI WA WATOTO. USICHAFUE. TUMIA
RASILIMALI VIZURI. REJESHA OILI ILIYOTUMIKA
KWENYE VITUO VYA KUKUSANYA.
Badilisha oili wakati injini bado ina joto baada ya
kuendeshwa, kama ifuatavyo:
1. Hakikisha jenereta iko kwenye eneo tambarare.
2. Ondoa kifuniko cha tundu (8, A) la kumwaga oili na
umwage oili yote ndani ya kontena inayofaa.
3. Rejesha kifuniko cha tundu (8, A) la kumwaga oili na
ukaze vizuri.
4. Legeza skrubu tatu za kifuniko (3) cha udumishaji na
uondoe kifuniko chakando cha udumishaji.
5. Safisha eneo linalozingira tundu la kujazia oili, ondoa
kifaa cha kupima kiwango cha oili na upanguse ukitumia
kitambaa safi.
6. Polepole weka oili iliyopendekezwa (takriban lita 1.0)
ndani ya tundu la kujazia oili (4). Acha ili kuruhusu oili
kutulia. Jaza hadi ifikie alama inayoonyesha imejaa (full)
(tundu la juu) kwenye kifaa cha kupima kiwango cha oili
(5, A).
7. Pangusa kifaa cha kupima kiwango cha oili kila mara
kiwango cha oili kinapokaguliwa. Usijaze kupita kiasi.
8. Rejesha kifaa cha kupima kiwango cha oili.
9. Pangusa oili yoyote iliyomwagika.
10. Rejesha kifuniko cha kando cha udumishaji na ukitumia
mkno ukaze skrubu tatu za kifuniko cha udumishaji.
BRIGGSandSTRATTON.COM

Hide quick links:

Tabla de contenido

Solución de problemas

loading

Este manual también es adecuado para:

030796-00

Tabla de contenido