Murray MP450D20 Manual Del Operador página 85

Cortacésped de empuje manual
Tabla de contenido
Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 20
8.1.2 Jinsi ya Kuzima injini
Mashine hii imewekewa na kidhibiti cha injini. Mfumo huu
hutumiwa kila wakati opereta anataka kusimamisha ubapa
kwa kuizima injini;
• Kuisimamisha injini (na ubapa), wachilia wengo ya
kudhibiti injini. Wengo itarudi kwa nafasi yake ya asili
ambayo inaizima injini moja kwa moja,
8.2 Kukata Nyasi
!
ONYO! Daima fuata taratibu za usalama wakati
unatumia mashine ya kukata nyasi. Soma kwa makini
maelekezo ya usalama kwa mwongozo huu kabla ya kuitumia
mashine ya kukata nyasi.
!
ONYO! Kabla uanze kukata nyasi, angalia wengo ya
injini ya kuwasha/kuzima mara kadhaa ili uwe na
uhakika ya kwamba inafanya kazi vizuri. Hakikisha kwamba
kebo ya nguvu inaweza kutumika vizuri (yaani haitingiki kwa
njia yoyote ile).
!
ONYO! Usiwahi fungua mlango wa nyuma, kifuniko ya
kifaa kinachotoa chaji kutoka kando wakati injini
inatumika. Majeraha makubwa yanaweza kusababishwa
kutokana na vitu vinavyoruka nje kutoka ndani ya deki!
8.2.1 Jinsi ya Kukata Nyasi - Ushauri Jumla
1. Kwa matokeo bora, kata nyasi wakati imekauka. Nyasi
nyevunyevu huziba makali na mfumo wa kukusanya nyasi..
2. Usiwahi tumia urefu wa kukata ulio chini kabisa ya kwa
mkato wa kwanza wa msimu au katika hali ya ukame.
3. Wakati unatumia mashine katika modi ya boji, hakikisha
kwamba uchafu wa nyasi unaweza kusambaratishwa vizuri
na kwa kuepuka kukata nyasi nyevunyevu au refu. Kwa ajili ya
kukata nyasi nyevunyevu au ndefu, simamisha mashine mara
kwa mara ili kusafisha ubapa na deki na kifaa kinachofaa
(usisafishe kwa kutumia mkono).
4. Chagua eneo la kukatwa.
5. Zingatia ardhi ya eneo na/au vikwazo.
6. Kwa ufanisi na kugeuka kidogo, kata katika laini moja, iliyo
sambamba, kwa mistari iliyo karibiana. Kutokana na hiyo, chagua
nafasi mwafaka ya kuanza kutoka na ulainishe mashine vizuri.
7. Chagua modi ya operesheni inayofaa (kukusanya kwa
mfuko wa nyuma, kutoa uchafu kutoka kando au aina ya boji
kama inafaa kwa modeli yako- Rejea kifungu cha 2. Vipengele
Maalum) na uitayarishe mashine kwa kufuata kifungu cha 7.2
Kuweke Modi Inayohitajika.
8.2.2 Jinsi ya Kukata Nyasi - Operesheni ya Mashine
1. Wakati mashine iko katika nafasi ya kuanza kukata, fuata
kifungu cha 8.1.1Jinsi ya Kuwasha Injini ili uiwashe kuanza
injini na mfumo kukata.
2. Shikilia mpini wa juu kwa nguvu na wengo ya kudhibiti injini
ikiwa imewekwa.
3. Anza kukata kwa kusongeza mashine mbele kwa kasi ya
kutembea:
Kwa modeli za kusukuma;
• Sukuma mashine mbele kupitia nyasi inayofaa kukatwa.
Kwa modeli zinazojiendesha;
• Fuata kifungu cha 8.2.3 Jinsi ya Kutumia Mbinu ya
Kujiendesha.
8.2.3 Jinsi ya Kutoa Uchafu kwa Mfuko Wa Nyasi
• Inatumika kwa modeli zilizo na Mfuko Wa Nyasi pekee
(ona Sehemu ya pili.
Wakati nyasi iliyokatwa inaanza kuambatana na mashine, ni
wakati wa kutoa uchafu kwa mfuko Wa nyasi.
!
KUMBUKA! Kabla ya kutoa mfuko wa nyasi, wachilia
wengo ya kudhibiti injini ili uisimamishe injini na ungoje
hadi ubapa umewacha kuzunguka kabisa.
1. Tumia mkono mmoja kuinua mlango wa nyuma na utumie
mkono mwingine kushikilia mpini wa mfuko wa kubebea nyasi
(ona Kielelezo.35)
2. Wakati uko mbali na mashine, wachilia mlango wa nyuma,
ili kuiruhusu irudi na kuifunga njia ya kuteremshia ya nyuma.
Kielelezo. 35
3. Mwaga nyasi iliyokatwa kutoka kwa mfuko wa nyasi.
4. Ambatisha mfuko wa nyasi kama ilivyoelezwa katika
sehemu ya 6.2 Kushikanisha Mfuko wa Nyasi.
!
KUMBUKA! Ili uhakikishe kwamba vipandikizi vya
nyasi vinaweza kukusanywa katika mfuko wa nyasi, njia
ya kuteremshia uchafu ya nyuma na ndani ya deki ya mashine
zinafaa kuzuiliwa kwa kuzibwa yoyote, kama vile kukusanyika
kwa uchafu wa nyasi. Usitumie mikono au miguu kutoa uchafu
wa nyasi kutoka eneo lolote la mashine. Kama kuna sehemu
imezibwa, tumia chombo kinachofaa kama brashi kuitoa.
8.2.4 Jinsi ya Kutumia Mbinu ya Kujiendesha (modeli ya
MX675RMD22H pekee)
Wakati mashine imetayarishwa kukata nyasi, na injini
inanguruma (weka wengo ya kudhibiti injini katika mpini wa
juu), sukuma polepole wengo ya kuendesha mbele dhidi ya
mbele dhidi ya mpini wa juu (ona Kielelezo.36).
Mashine itajisongeza mbele wakati wengo ya kujiendesha iko
katika nafasi hii.
Ili usimamishe mashine ikijisongeza, wachilia wengo ya
kujiendesha.
!
KUMBUKA! Tumia mbinu ya kujiendesha wakati
unakata nyasi katika laini zilizonyooka pekee; Hakikisha
umezima mbinu ya kujiendesha na urejelee mbinu ya
kudhibiti kwa kusukuma wakati unageuza.
Kielelezo.36
13
Tabla de contenido

Solución de problemas

loading

Tabla de contenido