Briggs & Stratton 110000 Manual Del Operario página 52

Ocultar thumbs Ver también para 110000:
Tabla de contenido
Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 16
1.
Toa mafuta kutoka kwenye injini. Angalia Ondoa Mafuta sehemu.
2.
Ondoa kichujio cha hewa (G, Kielelezo 15) na utupe kwa njia inayofaa.
3.
Kabla hujasakinisha kichujio kipya cha mafuta, lainisha kiasi kwa kifaa cha kichujio
cha mafuta kwa mafuta freshi na safi.
4.
Sakinisha kichujio cha mafuta kwa mkono hadi kifaa kisgusane na adapta ya kichujio
cha mafuta, kisha kaza kichujuio cha mafuta kwa mizunguko 1/2 hadi 3/4.
Ongeza mafuta. Angalia Ongeza Mafuta sehemu.
5.
6.
Washa na uendeshe injini. Wakati injini inachemka, kagua kwa uvujaji wa mafuta.
7.
Zima injini na uangalie kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi cha mafuta kiko juu ya
kiashiria kilichojaa (B, Kielelezo 16) kwenye kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta
kwenye kipimaji mafuta.
Badilisha Mafuta ya Injini
Hakikisha kuwa mtambo uko katika kiwango.
Safisha eneo la kujaza mafuta kutokana na uchafu wowote.
Tazama Vipimo Maalum sehemu ya uwezo wa mafuta.
1.
Ondoa kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 16) na upanguse kwa
kitambaa safi.
2.
Mwaga taratibu mafuta katika injini ya mafuta hadi ijae (C, Kielelezo 16). Usijaze
kupita kiasi. Baada ya kuongeza mafuta, subiri dakika moja na kisha uangalie
kiwango cha mafuta.
3.
Sakinisha na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 16).
4.
Ondoa kifaa cha kupima mafuta na ukague kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi cha
mafuta kiko juu ya kiashiria kilichojaa (B, Kielelezo 16) kwenye kifaa cha kuangalia
kiwango cha mafuta kwenye kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta.
5.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 16).
6.
Unganisha waya ya kiziba cheche (D, Kielelezo 12) kwenye kiziba cheche (E).
Shughulikia Kichuja Hewa
Tazama Kelelezo: 17, 18
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto haraka sana na kulipuka.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya moto au kifo.
Usiwashe na kuendesha kamwe wakati uunganishaji wa kisafisha hewa (iwapo kipo)
au kichuja hewa (iwapo kipo) kimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au majimaji yaliyoshinikizwa kusafisha kichujio. Hewa
iliyoshinikizwa inaweza kuharibu kichujio na majimaji yatayeyusha kichujio.
Angalia Ratiba ya Udumishaji kwa mahitaji ya huduma
Modeli mbalimbali zinatumia povu au kichujio cha karatasi. Baadhi ya modeli pia zinaweza
kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na kutumiwa
tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye injini yako na
ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Povu ya Hewa
1.
Fungua bizimu (A, Kielelezo 17).
2.
Ondoa kifuniko (B, Kielelezo 17).
3.
Ili kuzuia uchafu kutokana na kuanguka kwenye kabureta, kwa makini ondoa elementi
ya povu (C, Kielelezo 17) kutoka kwenye msingi wa kichujio cha hewa.
4.
Safisha elementi ya povu (C, Kielelezo 17) sabuni ya maji na maji. Finyiza ili kukausha
elementi ya povu kwenye kitambaa safi.
5.
Eneza elementi ya povu (C, Kielelezo 17) kwa mafuta safi ya injini. Ili kuondoa mafuta
ya ziada ya injini, finyiza elementi ya povu finyiza elementi ya povu kwenye kitambaa
safi.
6.
Sakinisha elementi ya povu (C, Kielelezo 17) juu ya msingi wa kichujio cha hewa.
7.
Sakinisha kifuniko (B, Kielelezo 17) na ufunike kwa (ki)vifuniko (A).
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Legeza bizimu (A, Kielelezo 18).
2.
Ondoa kifuniko (B, Kielelezo 18).
52
3.
Ili kuzia uchafu kutokana na kuangaka kwenyekabureta, kwa makini ondoa kisafishaji
cha mwanzo (D, Kielelezo 18) na kichujio (C) kutoka kwenye msingi wa kichujio cha
hewa.
4.
Ondoa kisafishaji cha kwanza (D, Kielelezo 18), ikiwa kipo, kutoka kwenye kichujio
(C).
5.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio (C, Kielelezo 18) kwenye sehemu
ngumu. Iwapo kichujio ni kichafu kupita kiasi, badilisha kwa kichujio kipya.
6.
Osha kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 18), ikiwa kipo, katika sabuni ya maji na
maji. Ruhusu kisafishaji cha mwanzo kukauka kabisa. Kamwe usiweke mafuta
kwenye kisafishaji cha mwanzo.
7.
Kusanya kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 18), ikiwa kipo, kwenye kichujio (C).
8.
Sakinisha kichujio (C, Kielelezo 18), na kisafishaji cha mwanzo (D), ikiwa kipo, kwenye
msingi wa kichujio cha hewa. Hakikisha kichujio hutoshea kwa usalama katika sehemu
ya chini ya kichuja hewa.
9.
Sakinisha kifuniko (B, Kielelezo 18) na ulinde kwa bizimu (A). Hakikisha bizimu
imekazwa.
Fanyia huduma Mfumo wa Mfuta
Tazama Kielelezo: 19
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto haraka sana na kulipuka.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au kifo.
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
Kagua njia za mafuta, tangi, kifuniko na sehemu zingine ili uone kama kuna nyufa
na uvujaji. Badilisha kama itahitajika.
Kabla ya kusafisha au kubadilisha kichujio cha mafuta , mimina mafuta kutoka kwa
tangi ya mafuta au au funga vali ya kuzuia mafuta.
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka pale ambapo yatavukiza kabla ya kuwasha injini.
Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa kwa namna sawa na
sehemu asili.
Kichujio cha Fueli, iwapo kipo
1.
Kabla ya kusafisha au kubadilisha kichujio cha fueli (A, Kielelezo 19), ondoa mafuta
kwenye tangi au funga vali ya kifuniko cha fueli. Vinginevyo, fueli inaweza kuvuja na
kusababisha moto au mlipuko.
2.
Tumia koleo kufinyiza vichupo (B, Kielelezo 19) kwenye vibanio (C), kisha telezesha
vibanio kutoka kwenye kichujio cha fueli (A). Zungusha na uvute tundu za fueli (D)
kutoka kwenye kichujio cha fueli.
3.
Angalia tundu za fueli (D, Kielelezo 19) kwa nyufa na uvujaji. Badilisha ikiwezekana.
4.
Badilisha kichujio cha fueli kwa kichujio asili cha kifaa cha ubadilishaji (A, Kielelezo
19).
5.
Linda tundu za fueli kwa vibanio (C) kama ilivyoonyeshwa (D, Kielelezo 19).
Shughulikia Mfumo wa Kupoesha
Onyo
Injini inayoendesha inazalisha joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa moto
zaidi.
Kuchomeka vikali kunaweza kusababishwa unapogusana nazo.
Uchafu unaoweza kuwaka, kama vile majani, nyasi, brashi, n.k., unaweza kushika
moto.
Ruhusu mafla, silinda na mapezi ya injini kupoa kabla ya kugusa.
Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
Notisi
Usitumie maji kusafisha injini. Maji yanaweza kuchafua mfumo wa fueli. Tumia
brashi au kitambaa kilichokauka kusafisha injini.
Hii ni injini inayopoeshwa na hewa. Uchafu unaweza kuzuia mtiririko wa hewa na
kusababisha injini kuchemka kupita kiasi, na kusababisha utendakazi mbaya na kupunguza
maisha ya injini.
1.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kuondoa uchafu kutoka kwenye grili ya
kuingiza hewa.
BRIGGSandSTRATTON.com
Tabla de contenido
loading

Este manual también es adecuado para:

120000

Tabla de contenido