Vanguard 25V000 Manual Del Operador página 49

Ocultar thumbs Ver también para 25V000:
Tabla de contenido
Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 16
Onyo
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo.
• Usiwashe washa na kuendesha injini kamwe wakati kifaa cha usafishaji hewa
(iwapo kipo) au chujio la hewa (iwapolipo) vimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio. Hewa
iliyoshinikizwa inaweza kuharibu chujio na maji yatayeyusha chujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji wa mahitaji ya huduma.
Chujio la Hewa la Karatasi
1.
Legeza sehemu za kufunga (C, Kielelezo 20).
2.
Ondoa kifuniko (A, Kielelezo 20).
3.
Ondoa chujio (B, Kielelezo 20).
4.
Ili kulegeza uchafu, gongesha chujio (B, Kielelezo 20) kwa utaratibu kwenye
eneo gumu. Ikiwa chujio ni chafu kupita kiasi, badilisha kwa chujio mpya.
5.
Sakinisha chujio (B, Kielelezo 20).
6.
Weka kifuniko (A, Kielelezo 20) na ufunge vizuri kwa sehemu za kufunga (C).
Hakikisha sehemu za kukazia zimekazwa kabisa.
Chujio la Hewa la Karatasi - Nyembamba
1.
Songeza wenzo (A, Kielelezo 21) ili kufungua kifuniko (C).
2.
Songeza sehemu za kufunga (B, Kielelezo 21) ili kuondoa kifuniko (C).
3.
Ondoa chujio (D, Kielelezo 21).
4.
Ili kulegeza vifusi, gongesha chujio (D, Kielelezo 21) kwa utaratibu kwenye eneo
gumu. Ikiwa chujio ni chafu kupita kiasi, badilisha kwa chujio mpya.
5.
Sakinisha chujio (D, Kielelezo 21).
6.
Sakinisha kifuniko (C, Kielelezo 21). Songeza wenzo (A) hadi eneo la kufunga.
Kumbuka: Kagua jinsi kifuniko cha foam (E, Kielelezo 21) kilivyotoshea. Hakikisha
kwamba kifuniko cha foam nimeingia vizuri mahali pake (F).
Fanyia huduma Mfumo wa Mfuta
Tazama Kielelezo: 22
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto haraka sana na kulipuka.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo.
• Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
• Kagua tundu za mafuta, tangi, kifuniko kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha
kama itahitajika.
• Kabla ya kusafisha au kubadilisha kichujio cha mafuta , mimina mafuta kutoka kwa
tangi ya mafuta au au funga vali ya kuzuia mafuta.
• Mafuta yakimwagika, subiri mpaka pale ambapo yatavukiza kabla ya kuwasha
injini.
• Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa kwa namna sawa na
sehemu asili.
Chujio Msingi la Mafuta, iwapo lipo
1.
Ondoa kifuniko cha mafuta (A, Kielelezo 22).
2.
Ondoa chujio msingi la mafuta (B, Kielelezo 22).
3.
Iwapo chujio msingi la mafuta ni chafu, lisafishe au ulibadilishe. Ukibadilisha chujio
msingi la mafuta, hakikisha umetumia chujio msingi la mafuta ambalo si ghushi.
Shughulikia Mfumo wa Kupoesha
Onyo
Injini inayoendesha inazalisha joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa
moto zaidi.
Kuchomeka vikali kunaweza kusababishwa unapogusana nazo.
Uchafu unaoweza kuwaka, kama vile majani, nyasi, brashi, n.k., unaweza
kushika moto.
• Ruhusu mafla, silinda na mapezi ya injini kupoa kabla ya kugusa.
• Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
Notisi
Usitumie maji kusafisha injini. Maji yanaweza kuchafua mfumo wa fueli.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kusafisha injini.
Hii ni injini inayopoeshwa na hewa. Uchafu unaweza kuzuia mtiririko wa hewa na
kusababisha injini kuchemka kupita kiasi, na kusababisha utendakazi mbaya na
kupunguza maisha ya injini.
1.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kuondoa uchafu kutoka kwenye grili ya
kuingiza hewa.
2.
Weka uhusiano, springi na vidhibiti safi.
3.
Weka ene lililo karibu na nyuma ya mafla, iwapo ipo, huru kutokana na uchafu
wowote unaoweza kuwaka.
4.
Hakikisha mapezi ya kupoesha mafuta, iwapo yapo, yako huru kutokana na
uchafu.
Baada ya kipindi cha muda, uchafu unaweza kukusanyika kwenye mapezi ya
kupoesha silinda na kusababisha injini kuwa moto kushinda kiasi. Uchafu huu hauwezi
kuondolewa bila kutokusanyika kwa kiasi fulani kwa injini. Ruhusu Mtoa Huduma wa
Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa kukagua na kusafisha mfumo wa kupoesha hewa
kama ilivyopendekezwa kwenye Ratiba ya Udumishaji.
Hifadhi
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya kuchomeka au kifo.
Wakati wa Kuhifadhi Mafuta Au Kifaa Kilicho na Mafuta Kwenye Tangi
• Hifadhi mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji, au vitu vingine ambavyo
vina taa za moto au vyanzo vya mwako kwa sababu vinaweza kuwasha moto
kwenye mvuke wa mafuta.
Mfumo wa Mafuta
Tazama Kielelezo: 23 
Hifadhi kiwango cha injini (mkao wa kawaida wa kuendesha). Jaza tangi la mafuta (A,
Kilelezo 23) kwa mafuta. Ili kuruhusu uvukizi wa mafuta, usijaze kupita chini ya shingo
ya tangi la mafuta (B). 
Mafuta yanaweza kuharibika yanapohifadhiwa katika kontena ya uhifadhi kwa zaidi ya
siku 30. Kila mara unapojaza kontena kwa mafuta, ongeza kiimarishaji mafuta kwenye
mafuta kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtengenezaji. Hii inafanya mafuta kukaa
yakiwa safi na kupunguza matatizo yanayohusiana na mafuta au uchafu katika mfumo
wa mafuta.
Si lazima umwage mafuta kutka kwenye injini wakati kiimarishaji mafuta kinapoongezwa
kama ilivyoagizwa. Kabla ya kuendesha, WASHA injini kwa dakika 2 ili kueneza mafuta
na kiimarishaji kote kwenye mfumo wa mafuta.
Ikiwa petroli ndani ya injini haijatibiwa kwa kiimarishaji mafuta, ni lazima imwagwe
kwenye kontena iliyoidhinishwa. Endesha injini hadi isimame kutokana na ukosefu wa
mafuta. Matumizi ya kiimarishaji mafuta kwenye kontena ya uhifadhi yanapendekezwa ili
kudumisha usafi. 
Mafuta ya Injini
Wakati injini bado ina joto, badilisha mafuta ya injini. Tazama sehemu Kubadilisha
Mafuta ya Injini.
Utafutatuzi
Kwa usaidizi, wasiliana na mhudumu wa karibu au nenda kwenye
VanguardEngines.com au piga 1-800-999-9333 (Marekani).
Maelezo
Muundo: 25V000 
Unyonyaji Mafuta 
Shimo 
Mpigo  
Kiwango cha Oili 
Pengo la Plagi ya Spaki 
Mkufu wa Plagi ya Spaki 
24.898 ci (408 cc) 
3.465 inchi (88 milimita) 
2.638 inchi (67 milimita) 
28 - 32 oz (,82 - ,95 L) 
.030 inchi (,76 milimita) 
170 lb-in (19.2 Nm) 
49
Tabla de contenido
loading

Tabla de contenido