QPT™ (QUIET POWER TECHNOLOGY™) Kielelezo
Kipengele hiki inaimarisha utumizi wa mafuta.
Wakati swichi ya QPT (W) IMEWASHWA, kasi ya
injini itaongezeka kadri vifaa vinavyotumia umeme
vinapounganishwa, na kupunguka kadri vifaa
vinavyotumia umeme vinapoondolewa.
Swichi ikiwa imezimwa, injini itanguruma kwa kasi zaidi.
Kurejesha Nishati Nyumbani kwa Kutumia
Swichi ya Ubadilishaji
Uunganishaji kwenye mfumo wa umeme wa nyumba
yako ni lazima utumie swichi ya ubadilisha isiyo otomatiki
iliyowekwa na fundi wa umeme aliyehitimu. Muunganisho
huu ni lazima utenganishe nishati ya jenereta na umeme
wa kawaida na uambatane na sheria na kanuni zote
husika za umeme.
Kurejesha Nishati kwa Kutumia Kebo Ndefu
Matumizi ya umeme ya jenereta hii, hayafai kupita uwezo
wa nguvu za umeme zilizopendekezwa, katika hali
iliyopendekezwa, kama ilivyoonyeshwa kwenye lebo ya
data ya kifaa. Punguza matumizi ya umeme unapotumia
jenereta katika hali ambazo hazijapendekezwa.
Tumia nyaya-enezi za ubora wa juu kuambatana na IEC
60245-4 na nyaya za kutoa umeme za kutoa umeme
wa AC kwenye jenereta za volti 230. Kagua nyaya-enezi
kabla ya kila tumizi. Hakikisha kwamba nyaya-enezi zote
zina vipimo mwafaka na hazijaharibika. Unapotumia
nyaya-enezi chini ya 40° C, jumla ya urefu wa nyaya kwa
sehemu ya msalaba ya 1.5 mm² haifai kuzidi mita 50 au
kwa sehemu ya msalaba ya 2.5 mm² haifai kuzidi mita
80.
ONYO! Nyaya-enezi zilizozidisha kiwango cha
vitumizi zinaweza kupata joto kubwa, kupinda,
na kuchomeka na kusababisha kifo au majeraha
mabaya.
• Vifaa vya elektroniki, pamoja na kebo na vizibo vya
kuunganisha, havifai kuwa na hitilafu.
1. Weka ving'ora vya kaboni monoksidi.
2. Unapoendesha jenereta ukitumia kebo ndefu,
hakikisha ipo mahali wazi, nje, angalau mita
6.1 mabla na mahali kuna watu na ekzosi ikiwa
umeelekezwa mbali.
3. Kebo ndefu zinazoelekea moja kwa moja hadi
ndani ya nyumba, na kuendesha vifaa vya ndani ya
nyumba HAIPENDEKEZWI.
ONYO! Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi,
gesi ya sumu ambayo inaweza kukuua kwa
dakika chache. Hauwezi kuinusa, kuiona, wala
kuionja. Hata kama huwezi kunusa mafukizo
yanayotolewa, bado unaweza kupumua gesi ya
monoksidi ya kaboni.
• Kebo ndefu zinazoelekea moja kwa moja hadi ndani ya
nyumba zinaongeza hatari kwako ya sumu ya kaboni
monoksidi kupitia mianya.
• Iwapo kebo ndefu inayoelekea moja kwa moja hadi
ndani ya nyumba inatumika kuendesha vifaa vya
umeme vilivyo ndani ya nyumba, mwendeshaji
anatambua kwamba hili linaongeza hatari ya sumu ya
CO kwa watu walio ndani ya nyumba na anawajibikia
hatari hiyo.
4. Weka swichi ya ubadilishaji isiyo otomatiki punde
1
iwezekanavyo iwapo jenereta itatumiwa kurejesha
nishati nyumbani.
Plagi za Volti 230 za AC Kielelezo
Tumia plagi (M) ili kuendesha Volti 230 za AC, msururu
mmoja, 50 Hz ya vitumizi vya umeme. Plagi zinalindwa
kutokana na uzito kwa kutumia swichi za kukata umeme
za kusukuma ili kuweka upya (N).
Ulinzi wa vifaa vya umeme unategemea swichi za kukata
umeme zinazoafikiana na jenereta. Badilisha swichi
ya kukata umeme na ile yenye kadirio la sifa sawia za
utendakazi.
ONYO! Volti za jenereta zinaweza
kusababisha mshtuko wa umeme au
kuchomeka kunakoweza kusababisha
kifo au majeraha mbaya.
• Usiguze nyaya au plagi zilizo wazi.
• Usitumie jenereta yenye nyaya za umeme ambazo
zimechakaa, kuchubuka, wazi au vinginevyo
zilizoharibika.
• Usitumie jenereta kwenye mvua au wakati kuna
unyevunyevu.
• Usishike jenereta au nyaya za umeme ukiwa
umesimama ndani ya maji, ukiwa miguu mitupu ama
mikono na miguu ikiwa na maji.
• Usiruhusu watu ambao hawajahitimu au watoto
kuendesha au kuhudumia jenereta.
• Weka watoto mahali salama mbali na jenereta.
Plagi za Volti 12 za DC Kielelezo
Umeme wa upeo unaopatikana kwenye plagi ya Volti
12 (T) ni Amp 5. Kikata mkondo cha DC kinalinda plagi
hii kutokana na matumizi kupita kiasi. Matumizi kupita
kiasi yakitokea, kikata mkondo (R) kitazima (kitufe cha
kubonyezwa kitachomoza nje). Subiri dakika chache na
ubonyeze kitufe ndani ili kuweka upya kikata mkondo.
Vituo vya USB vya Volti 5 za DC
Umeme wa upeo unaopatikana kwenye vituo vya
USB (V) ni Amp 2.1 kwa Volti 5. Kipenyo cha USB
kinakuruhusu kuchaji chombo chochote kinachotumia
USB ukitumia waya ya kuchaji ya USB (haijajumuishwa
na kifaa).
ILANI Ili kupata matokeo bora zaidi unapochaji vifaa
vya, tumia kituo cha USB cha chini.
ILANI Ya kuchaji ITE (Kifaa cha Teknolojia ya Maelezo)
pekee.
King'ora cha Matumizi Kupita Kiasi
Taa nyekundu ya kiashirio (B) inawaka na kukata umeme
kwa plagi ukitumia kupita kiasi. Taa ya kijani ya kiashirio
cha kuzalisha pia itazima. Ikiwa jenereta ilitumika kupita
kiasi, ni lazima uzime na uondoe vipengee vyote vya
kiumeme, kisha ubonyeze kitufe kikuu cha uwekaji upya
cha jenereta ili kuendelea katika matumizi.
Kiashirio cha Uzalishaji
Taa ya kijani ya kiashiria (C) inawaka wakati jenereta
inafanya kazi kawiada.
1
1
Kielelezo
1
Kielelezo
6
Kielelezo
6
7