6. Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo
5) na ukague kiwango cha oili. Inafaa iwe kwenye alama
inayoonyesha IMEJAA (FULL) (B) iliyo kwenye kifaa cha
kupima kiwango cha oili.
7. Ikiwa IMEJAA (FULL), ingiza kifaa cha kupimia kiwango
cha oili na ukaze vizuri.
8. Ikiwa CHINI (LOW), ongeza oili polepole ndani ya kopo
la kujazia oili ya injini (C ) . Usijaze kupita kiasi. Baada
ya kuongeza oili, subiri dakika moja na kisha ukague
kiwango cha oili.
Kumbuka: Usiongeze oili kupitia tundu la kumwaga oili kwa
haraka, (ikiwa lipo).
9. Funika na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili.
Shinikizo la Oili
Ikiwa shinikizo la oili liko chini sana, swichi ya shinikizo
(ikiwa ipo) itazima injini au kuwasha kifaa cha onyo kwenye
kifaa. Hili likifanyika, zima injini na ukague kiwango cha oili
ukitumia kijiti cha kupima oili.
Ikiwa kiwango cha oili kiko chini ya alama inayoonyesha
ONGEZA (ADD), ongeza oili hadi ifikie alama inayoonyesha
IMEJAA (FULL). Washa injini na ukague shinikizo linalofaa
kabla ya kuendelea kuendesha.
Ikiwa kiwango cha oili kiko kati ya alama inayoonyesha
ONGEZA (ADD) na ile inayoonyesha IMEJAA (FULL),
usiwashe injini. Wasiliana na muuzaji aliyeidhinishwa ili
kurekebisha tatizo la shinikizo la oili.
Ongeza Mafuta
Mafuta ni lazima yatimize mahitaji haya:
• Petroli safi, freshi, isiyo na risasi (unleaded).
• Kiwango cha chini zaidi cha okteni 87 / 87 AKI (91
RON). Kwa matumizi ya maeneo ya nyanda za juu,
tazama hapa chini.
• Petroli iliyo na hadi ethanoli 10% (gasoholi) inakubalika.
Notisi Usitumie petroli ambayo haijaidhinishwa, kama
vile E15 na E85. Usichanganye oili kwenye petroli au
kurekebisha injini ili itumie mafuta mbadala. Matumizi ya
mafuta ambayo hayajaidhinishwa yatasababisha uharibifu
wa vipengele vya injini, jambo ambalo halijasimamiwa na
hakikisho.
Ili kulinda mfumo wa mafuta kutokana na utengenezaji wa
gundi, changanya kiimarishaji mafuta ndani ya mafuta.
Tazama Hifadhi. Mafuta yote si sawa. Iwapo matatizo ya
kuwasha au utendakazi yatatokea, badilisha unakonunua
mafuta au ubadilishe aina. Injini hii imeidhinishwa
kuendeshwa kutumia petroli. Mfumo wa kudhibiti mafukizo wa
injini hii ni EM (Engine Modifications (Marekebisho ya Injini)).
Mahitaji ya Maeneo Yaliyo Juu:
• Katika minuko zaidi ya fiti 5,000 (mita 1,524), kiwango
cha chini cha okteni 85//85 AKI (89 RON) cha petroli
kinakubalika.
• Kwa injini iliyo na kabureta, marekebisho ya mwinuko wa
juu yanahitajika ili kudumisha uambatanaji na sera ya
mafukizo. Uendeshaji bila marekebisho haya unaweza
kusababisha kupunguka kwa utendakazi, matumizi ya
70
mafuta kuongezeka, na mafukizo kuongezeka. Wasiliana
na Mtoa Huduma wa Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa
kwa maelezo ya marekebisho ya mwinuko wa juu.
• Uendeshaji injini katika mwinuko wa chini ya fiti
2,500 (mita 762) na marekebisho ya mwinuko wa juu
hayapendekezwi.
• Kwa injini za Uingizaji Mafuta wa Kielektroniki (EFI),
hakuna marekebisho ya mwinuko wa juu yanahitajika.
Onyo
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka
kwa haraka sana. Kuwa mwangalifu sana unaposhughulikia
mafuta.
Kukosa Kuzingatia maagizo haya ya usalama kunaweza
kusababisha moto au mlipuko ambao unaweza kupelekea
majeraha mabaya ya kuchomeka au kifo.
Wakati wa Kuongeza Mafuta
• Zima injini na uache injini ipoe kwa angalau dakika 3
kabla ya kuondoa kifuniko cha mafuta.
• Zima sigara zote, biri, viko, na vyanzo vingine vya
mwako.
• Jaza tangi la mafuta nje au katika eneo lenye hewa
nyingi safi.
• Usijaze tangi la mafuta kupita kiasi. Ili uruhusu uvukizi
wa mafuta, usijaze hadi juu ya chini ya shingo la tangi
la mafuta.
• Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za
gesi, joto, na vyanzo vingine vya mwako.
• Kagua tundu za mafuta, tangi, kifuniko kama kuna
nyufa na uvujaji. Badilisha kama itahitajika.
• Mafuta yakimwagika, subiri mpaka pale ambapo
yatavukiza kabla ya kuwasha injini.
• Tumia tu kontena za petroli zilizoidhinishwa.
1. Safisha kifuniko cha mafuta kutokana na uchafu na vifusi.
2. Ondoa kifuniko cha mafuta (A, Kielelezo 6). Tazama
sehemu ya Vipengele na Vidhibiti.
3. Jaza tangi la mafuta (B) kwa mafuta. Ili uruhusu uvukizi
wa mafuta, usijaze hadi juu ya chini ya shingo la tangi la
mafuta (C).
4. Weka upya kifuniko cha mafuta.