Briggs & Stratton VANGUARD 10V000 Manual Del Operador página 53

Ocultar thumbs Ver también para VANGUARD 10V000:
Tabla de contenido
Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 24
Badilisha Oili ya Injini
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Ukimwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la
mafuta liwe tupu. Ikiwa si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto
au mlipuko.
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
Oili iliyotumika ni bidhaa taka na hatari na ni lazima itupwe kwa njia sahihi. Usitupe
pamoja na taka ya nyumbani. Wasiliana na mamlaka yako ya ndani, kituo cha huduma
au muuzaji ili kupata zana salama za kutupa au kutumia tena.
Kwa miundo ya Just Check & Add
, hauhitaji kubadilisha oili. Ikiwa unahitaji
kubadilisha oili, basi fuata utaratibu ufuatao.
Ondoa Oili
1.
Injini ikiwa imezimwa lakini ina joto, tenganisha waya wa plagi ya spaki (D,
Kielelezo 21) na uiweke mbali na plagi ya/za spaki (E).
2.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 22).
3.
Injini ina matundu mawili ya kumwaga oili (H, F, Kielelezo 23). Ondoa vifuniko vya
matundu ya kumwaga oili (H, F). Mwaga oili katika kontena iliyoidhinishwa.
4.
Weka na ukaze vifuniko vya tundu la kumwaga oili (H, F, Kielelezo 23).
Ongeza Oili
Hakikisha injini haijainama.
Safisha vifusi vyote kutoka kwenye eneo la kujazia oili.
Rejelea sehemu ya Vipimo ili kujua kiwango cha oili.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili. Rejelea sehemu ya Kuondoa Oili.
1.
2.
Polepole ongeza oili kwenye tundu la kujazia oili ya injini (C, G, Kielelezo 24).
Usiongoze oili nyingi kupita kiasi.
3.
Subiri dakika moja, na kisha, ukague kiwango cha oili.
4.
Weka kifaa cha kupima kiwango cha oili.
5.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Kiwango sahihi cha oili
kiko juu ya alama inayoashiria kujaa kwenye kifaa cha kupima kiwango cha oili.
Rejelea sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
6.
Weka na ukaze tena kifaa cha kupima kiwango cha oili.
7.
Unganisha waya wa plagi ya spaki kwenye plagi ya/za spaki. Rejelea sehemu ya
Kuondoa Oili.
Badilisha Oili ya Upunguzaji Gia
Baadhi ya injini zimewekwa Kifaa cha Upunguzaji Gia. Iwapo kipo, rejelea hatua za
mojawapo ya Vifaa vya Upunguzaji Gia vifuatavyo.
Kifaa cha Upunguzaji Gia kwa Uwiano wa 2:1
Ikiwa injini ina kifaa cha upunguzaji nyororo kwa uwiano wa 2:1 (G, Kielelezo 25), basi
hauhitaji kubadilisha oili. Oili katika injini pia inalainisha lifaa cha upunguzaji nyororo.
Kifaa cha Upunguzaji Klachi Oevu kwa Uwiano wa 2:1
Iwapo injini yako imewekwa kifaa cha upunguzaji klachi oevu kwa uwiano wa 2:1,
chukua hatua zifuatazo:
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 26).
2.
Ondoa plagi ya kumwaga oili (B, Kielelezo 26), na umwage oili ndani ya kontena
iliyoidhinishwa.
3.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwaga oili (B, Kielelezo 26).
4.
Polepole weka oili kwenye tundu la kujazia oili (C, Kielelezo 26). Tazama sehemu
ya Vipimo.
5.
Weka kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 26).
6.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 26) na ukague kiwango cha
oili. Kiwango sahihi cha oili kiko juu ya alama inayoashiria kujaa (B) kwenye kifaa
cha kupima kiwango cha oili.
7.
Weka kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 26).
Kifaa cha Upunguzaji Gia kwa Uwiano wa 6:1
Iwapo injini yako imewekwa kifaa cha upunguzaji gia kwa uwiano wa 6:1, chukua hatua
zifuatazo:
1.
Ondoa kifuniko cha tundu la kujazia oili (A, Kielelezo 27) na kifuniko cha kiwango
cha oili (B).
2.
Ondoa kifuniko cha tundu la kumwaga oili (C, Kielelezo 27) na umwage oili ndani ya
kontena iliyoidhinishwa.
3.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwaga oili (C, Kielelezo 27).
4.
Polepole weka oili (80W-90) ya upunguzaji gia ndani ya shimo la kujazia oili (D,
Kielelezo 27). Endelea kuongeza oili (80W-90) ya upunguzaji gia mpaka oili oili
ifurike kwenye shimo la kiwango cha oili (E).
5.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kiwango cha oili (B, Kielelezo 27).
6.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kujazia oili (A, Kielelezo 27).
KUMBUKA: Kifuniko cha tundu la kujazia oili (A, Kielelezo 27) kina shimo ndogo
(F) la kupitishia hewa na ni lazima liwekwe upande wa juu wa kifuniko cha gia kama
ilivyoonyeshwa.
Kufanya Udumishaji kwenye Chujio la Hewa
ONYO 
Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana. Moto au
mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Usiwashe na kuendesha injini kamwe wakati kifaa cha usafishaji hewa (iwapo
kipo) au chujio la hewa (iwapolipo) kimeondolewa.
NOTISI 
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio. Hewa iliyoshinikizwa inaweza
kuharibu chujio na vioevu vitayeyusha chujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji ili kujua mahitaji ya huduma.
Miundo tofauti itatumia vichujio vya sifongo au karatasi. Baadhi ya miundo pia iinaweza
kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na kutumiwa
tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye injini yako
na ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Legeza sehemu za kufunga (C, Kielelezo 28).
2.
Ondoa kifuniko (A, Kielelezo 28) na chujio (B).
3.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gongesha chujio (B, Kielelezo 28) kwenye eneo
gumu. Ikiwa chujio ni chafu, badilisha kwa chujio jipya.
4.
Weka chujio (B, Kielelezo 28).
5.
Weka kifuniko (A, Kielelezo 28) na ufunge vizuri ukitumia sehemu za kufunga (C).
Hakikisha sehemu za kufunga zimekazwa kabisa.
Chujio la Hewa la Karatasi - Nyembamba
1.
Sogeza wenzo (A, Kielelezo 29) ili kufungua kifuniko (C).
2.
Sogeza sehemu za kufunga (B, Kielelezo 29) ili kuondoa kifuniko (C).
3.
Ondoa chujio (D, Kielelezo 29).
4.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gongesha chujio (D, Kielelezo 29) kwenye eneo
gumu. Ikiwa chujio ni chafu, badilisha kwa chujio jipya.
5.
Sakinisha chujio (D, Kielelezo 29).
6.
Sakinisha kifuniko (C, Kielelezo 29). Songeza wenzo (A) hadi eneo la kufunga.
KUMBUKA: Kagua jinsi kifuniko cha sifongo (E, Kielelezo 29) kilivyotoshea. Hakikisha
kwamba kifuniko cha sifongo kimeingia vizuri mahali pake (F).
Kufanyia Huduma Mfumo wa Mafuta
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na
mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka yakauke kabla ya kuwasha injini.
Chujio la Mafuta, iwapo lipo
1.
Ondoa kifuniko cha mafuta (A, Kielelezo 30).
2.
Ondoa chujio la mafuta (B, Kielelezo 30).
3.
Iwapo chujio msingi la mafuta ni chafu, lisafishe au ulibadilishe. Ukibadilisha chujio
msingi la mafuta, hakikisha umetumia chujio msingi la mafuta ambalo si ghushi.
Hifadhi
Mfumo wa Mafuta
Rejelea Kielelezo:  31.
53
Tabla de contenido
loading

Este manual también es adecuado para:

Vanguard 12v000Vanguard 25v000

Tabla de contenido