ONYO
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi, gesi ya
sumu ambayo inaweza kukuua kwa dakika chache. Ingawa hauwezi kunusa
mafukizo yanayotolewa, bado unaweza kuvuta gesi hatari ya monoksidi ya
kaboni. Ukihisi mgonjwa, kizunguzungu, au mchovu unapotumia bidhaa hii,
nenda kwenye eneo lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa
umeathiriwa na sumu ya kaboni monoksidi.
•
Gesi ya kaboni monoksidi inaweza kujikusanya katika maeneno yenye watu. Ili
kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi, tumia bidhaa hii TU nje na mbali
na madirisha, milango na matundu.
•
Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa kaboni monoksidi vinavyotumia betri
pamoja na hifadhi ya betri kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtengenezaji.
Ving'ora vya moshi haviwezi kutambua gesi ya kaboni monoksidi.
•
USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi,
ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Baada ya kuendesha
bidhaa hii, gesi ya kaboni monoksidi inaweza kukusanyika kwa haraka katika
maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa kadhaa.
•
KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unaelekea na uelekeze
ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu.
NOTISI
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji vifaa
huenda waliongeza oili kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya kwanza,
hakikisha umekagua kiwango cha oili ni sahihi. Ongeza oili kama ilivyobainishwa na
maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, injini itaharibika na haiwezi
kukarabatiwa chini ya waranti.
KUMBUKA: Baadhi ya injini na vifaa vina vidhibiti vya mbali. Rejelea mwongozo wa
kifaa ili utambue mahali ambapo vidhibiti vya mbali viko na jinsi ya kuvitumia.
1.
Kagua oili ya injini. Tazama sehemu ya Kuangalia Kiwango cha Oili.
2.
Hakikisha kwamba vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo, vimezimwa.
3.
Geuza swichi ya kuzima (A, Kielelezo 7), iwapo ipo, hadi kwenye eneo
linaloonyesha WASHA.
4.
Sogeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 7), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
5.
Sogeza kidhibiti choki (C, Kielelezo 7) kwenye eneo linaloonyesha IMEFUNGWA.
KUMBUKA: Kwa kawaida choki haihitajiki wakati wa kuwasha upya injini iliyochemka.
6.
Sogeza vali ya kufunga mafuta (A, Kielelezo 7), iwapo ipo, hadi kwenye eneo
linaloonyesha FUNGUA.
7.
Kwa uthabiti shikilia kishikilio cha kamba ya kianzishaji (E, Kielelezo 7). Vuta
kishikio cha kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi ugumu, kisha vuta kwa
haraka.
ONYO
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka) kutavuta
mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia. Inaweza kupelekea
mifupa kuvunjika, michubuko au kuteguka maungo. Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka
wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na
kisha uvute haraka.
8.
Baada ya injini kuzima, sogeza vali ya kufunga mafuta (A, Kielelezo 7), iwapo ipo,
hadi kwenye eneo linaloonyesha IMEFUNGWA.
KUMBUKA: Injini ikikosa kuwasha baada ya majaribio 2 au 3, nenda kwenye
BRIGGSandSTRATTON.COM au upige simu kwa nambari 1-800-444-7774 (nchini
Marekani).
Zima Injini
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
•
Usikabe kabureta (iwapo ipo) ili kusimamisha injini.
1.
Swichi ya Kuzima, iwapo ipo: Sogeza swichi ya kuzima (A, Kielelezo 8) hadi
kwenye eneo linaloonyesha ZIMA.
Kidhibiti Injini, iwapo kipo: Songeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 8) hadi kwenye
2.
eneo linaloonyesha POLEPOLE na kisha kwenye eneo linaloonyesha SIMAMA.
3.
Baada ya injini kuzima, sogeza vali ya kufunga mafuta (D, Kielelezo 8), iwapo ipo,
hadi kwenye eneo linaloonyesha IMEFUNGWA.
Udumishaji
Maelezo ya Udumishaji
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Wakati wa huduma ya udumisha ikiwa ni muhimu kuinamisha kifaa, ikiwa tangi la
mafuta limeshikana na injini, hakikikisha kwamba ni tupu na upande wa plagi ya spaki
uko juu. Ikiwa tangi la mafuta si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au
mlipuko. Ikiwa injini imeinama katika mkao tofauti, haitaguruma kwa urahisi kwa sababu
ya kuchafuka kwa chujio la hewa au plagi ya spaki kwa oili au mafuta.
ONYO
Mwako wa injini usiokusudiwa unaweza kusababisha mshtuko wa umeme, moto
au mlipuko na kupelekea kunaswa, kukatwa kwa viungo kwa kiwewe, au majeraha
mabaya ya ukataji wa ngozi.
Kabla ya kufanya marekebisho au ukarabati:
•
Tenganisha nyaya zote za plagi ya spaki na uziweke mbali na plagi za spaki.
•
Tenganisha betri katika kichwa cha hasi (injini tu zenye kianzishaji cha umeme).
•
Tumia zana sahihi pekee.
Unapokagua uwepo wa cheche:
•
Tumia kifaa kilichoidhinishwa cha kujaribu plagi ya spaki.
•
Usikague cheche huku plagi ya spaki ikiwa imeondolewa.
ONYO
Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawa na ziwekwe katika eneo sawa
kama sehemu asilia. Sehemu nyingine huenda zinaweza kuharibu kifaa au kusababisha
majeraha.
NOTISI
Vijenzi vyote vilivyotumiwa kutengeneza injini hii ni lazima visalie kwenye maeneo yake
ili kupata uendeshaji bora.
Mwone Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kupata huduma zote za
udumishaji na kufanyia huduma injini na sehemu za injini.
Ratiba ya Udumishaji
Saa 5 za Kwanza
•
Badilisha oili.
Mpishano wa Saa 8 au Kila Siku
•
Kagua kiwango cha oili ya injini.
•
Safisha maeneo yaliyo karibu na mafla na vidhibiti.
•
Safisha grili ya kuingiza hewa.
Mpishano wa Saa 25 au Kila Mwaka
•
1
Safisha chujio la hewa
.
•
Safisha kisafishaji cha mwanzo, iwapo kipo.
Mpishano wa Saa 50 au Kila Mwaka
•
Badilisha oili ya injini.
•
Fanyia huduma mfumo wa ekzosi.
Kila Mwaka
•
Badilisha plagi ya/za spaki.
•
Badilisha chujio la hewa.
•
Badilisha kisafishaji cha mwanzo, iwapo kipo.
•
Fanyia huduma mfumo wa kupoesha
1
Safisha mara nyingi zaidi katika mazingira ya vumbi au wakati kuna vipengee vingi
hewani
Huduma ya Udhibiti wa Mafukizo
Ili kupata huduma ya udumishaji, ubadilishaji, au ukarabati wa vifaa na mifumo
ya kudhibiti mafukizo, wasiliana na kituo chochote kinachohitimu cha kukarabati
injini au mtoa huduma aliyehitimu wa kukarabati injini. Hata hivyo, ili kupata
huduma ya kudhibiti mafukizo ya "bila malipo", ni lazima kazi ifanywe na muuzaji
aliyeidhinishwa na kiwanda. Rejelea Kauli za Udhibiti Mafukizo.
1
49