Hatua ya 4: Kuunganisha Vitumizi vya
Umeme Mchoro
1
Matumizi ya umeme ya jenereta hii, hayafai kupita uwezo
wa nguvu za umeme zilizopendekezwa, katika hali
iliyopendekezwa, kama ilivyoashiriwa kwenye lebo ya
data ya kifaa. Punguza matumizi ya umeme unapotumia
jenereta katika hali ambayo haijapendekezwa.
Tumia nyaya-enezi za ubora wa juu kuambatana na IEC
245-4 na vitoleo vya volti 230 vya mkondo geuzi (AC)
vya jenereta pekee. Kagua nyaya-enezi kabla ya kila
tumizi. Hakikisha nyaya-enezi zote zina vipimo mwafaka
na hazijadhurika. Unapotumia nyaya-enezi chni ya 40° C,
jumla ya urefu wa nyaya kwa sehemu ya msalaba ya 1.5
mm² isizidi m 50 ama kwa sehemu ya msalaba ya 2.5
mm² isizidi m 80.
ONYO! Nyaya-enezi zilizopitisha kiasi cha vitumizi
zaweza kupata joto kubwa, kupinda, na kuchomeka
zikisababisha kifo ama majeraha makubwa.
• Vifaa vya umeme mkiwemo nyaya na plagi unganishi
hazitakiwi kuwa na kasoro.
230 Volt AC Kifaa cha Kupokea
Tumia kifaa cha kupokea (R) ili kutumia volti AC 230,
kwa awamu moja, 50 Hz kwa uzito wa electroniki.
Chombo cha kutumika kinafaa kulindwa kutokana na
uzito kwa kushinikiza upya mzunguko wa wimbi (K).
Ulinzi wa sehemu za elektroniki untagemea mizunguko
ya mawimbi ambayo yanaendana hasa kwa jenereta.
Badilisha mzunguko wa mawimbi na nyingine ya
kufanana na pia sifa za utendaji kazi wa kufanana.
ONYO! Nguvu za volti za jenereta zaweza
kusababisha mshtuko wa umeme au kuchoma
ama kusababisha kifo au majeraha makubwa.
• Usiguse nyaya zilizo uchi ama plagi.
• Usitumie jenereta na nyaya za umeme zilizoharibika,
kuzeeka, zilizo uchi ama kuharibika.
• Usitumie jenereta katika mvua ama hali ya unyevu.
• Usitumie jenereta kama umesimama kwa maji, ukiwa
miguu mitupu, ama miguu na mikono ikiwa na maji.
• Usiwakubalie watu wasiohitimu ama watoto ktumia
ama kutengeneza jenereta.
• Weka watoto kwa umbali salama kutoka kwa jenereta.
Kipokezi cha DC cha Volti 12
Upeo wa wimbi linalopatikana kwa kipokezi cha DC
cha volti 12 (G) ni wati 60 (Ampea 5). Kikatizaji cha
saketi cha DC (H) hulinda kipokezi hiki dhidi ya umeme
unaopita kiasi. Ikiwa umeme utapita kiasi, kikatizaji
cha saketi kitawaka (swichi ya kusukuma itachomoka).
Subiri dakika chache na usukume swichi ndani ili uweke
kikatizaji cha saketi upya.
Kipokezi hiki pamoja na adapta ya USB hukuwezesha
kuchaji kifaa chochote cha USB ukitumia kebo ya kuchaji
ya USB (haikuji na kifaa).
ILANI Kwa kuchaji ITE (Kifaa cha Teknolojia ya Taarifa)
pekee.
ILANI Wakati unatumia kipokezi hiki, sukuma swichi ya
QPT kwenye nafasi ya ZIMA (0).
Paneli ya LED Kielelezo
Kiashirio cha Uzalishaji
Taa ya kiashiria ya kijani ya LED huwaka wakati jenereta
infanya kazi sawasawa. Huashiria kwamba jenereta
inazalisha umeme na kupokeza plagi.
Kiashirio cha Uzito
Taa nyekundu ya kiashirio cha uzito cha LED huwaka na
kukata umeme kwa plagi kama unazidisha uzito. Taa ya
kiashirio cha kuzalisha ya kijani pia itazima. Sharti uzime
na kuchomoa plagi za vitumizi vyote vya umeme, kubofya
kitufe cha "Reset" halafu uchomeke plagi za umeme moja
kwa moja ili kuendeleza hali ya kawaida ya kazi.
Kiashirio cha Oili Kidogo
Mfumo wa Kiashirio cha Oili Kidogo umeundwa ili kuzuia
uharibifu wa mtambo unaosababishwa na kiwango cha chini
cha oili katika injini. Iwapo kiwango cha oili kimepungua zaidi
ya kipimo kilichowekwa, taa ya Kiashirio cha Oili Kidogo ya
manjano inawaka na kitufe cha kiwango cha oili kitazima
mtambo. Iwapo mtambo utazima ama taa ya njano ya
Kiashirio cha Oili Kidogo iwake unapovuta mpini-nywea,
angalia kiwango cha oili katika injini.
Uendeshaji Sambamba
Jenereta mbili fudukizi za Briggs & Stratton zinaweza
kuendesha sambamba kwa kutumia kifaa cha uendeshaji
sambamba cha Briggs & Stratton (kifaa cha hiari).
Wakati zinaendeshwa sambamba, jumla ya nishati
inayozalishwa inaonyeshwa katika chati.
Modeli
P2200 & P2200
P2200 & P3000
P3000 & P3000
ILANI Jumla ya umeme wa kielektroniki uliounganishwa
kwenye kifaa cha uendeshaji sambamba haufai kuzidi
upeo wa nashati inayozalishwa.
Pitia laha ya maelekezo ya vifaa vya uendeshaji
sambamba kwa maelekezo kamili kuhusu ufungaji na
uendeshaji wa jenereta zilizounganishwa.
Hatua ya 5: Uzimaji wa Jenereta
1. Zima na kutoa plagi za vitumizi vyote kutoka kwa
ubao wa plagi wa jenereta. Usizime mtambo kama
plagi za vifaa vitumizi havijazimwa wala kung'olewa.
2. Acha mtambo uwake bila vitumizi kwa dakika moja
ili kuimarisha hali ya joto ndani ya injini na jenereta.
3. Bofya swichi ya mtambo katika hali ya OFF (0) kuzima.
7
Upeo wa Zao
Wati 3000
Wati 3000
Wati 4800
7