7.
Kusanya kisafishaji cha mwanzo kilichokauka (D, Kielelezo 12, 13), ikiwa kipo,
kwenye kichujio (C).
8.
Sakinisha kichujio (C, Kielelezo 12, 13) na kisafishaji cha mwanzo (D), iwapo kipo,
katika eneo la kichujio (E) na usukume chini hadi kichujio kisonge kwenye nafasi.
9.
Sakinisha kifuniko cha kichujio cha hewa (B, Kielelezo 12, 13) na ulinde kwa
bizimu (A). Hakikisha bizimu imekazwa.
Fanyia huduma Mfumo wa Mafuta
Tazama Kielelezo: 14
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo.
• Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
• Kagua njia za mafuta, tangi, kifuniko na sehemu nyingine mara kwa mara ili uone
kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha kama itahitajika.
• Kabla ya kusafisha au kubadilisha kichujio cha mafuta, mimina mafuta kutoka kwa
tangi ya mafuta au ufunge vali ya kuzuia mafuta.
• Mafuta yakimwagika, subiri mpaka pale ambapo yatavukiza kabla ya kuwasha
injini.
• Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa kwa namna sawa na
sehemu asili.
Kichujio cha Mafuta, iwapo kipo
1.
Kabla ya kubadilisha kichujio cha mafuta (A, Kielelezo 14), iwapo kipo, mimina
mafuta kutoka kwa tangi la mafutai au funga vali ya kuzuia mafuta . La sivyo,
mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au mlipuko.
2.
Tumia koleo kubana vichupo (B, Kielelezo 14) kwenye vibanio (C), ) kisha
telezesha vibanio kutoka kwenye kichujio cha fueli (A). Zungusha na uvute njia za
mfuta (D) kutoka kwenye kichujio cha mafuta.
3.
Kagua njia za mfuta (D, Kielelezo 14)ili uone kamakuna nyufa au uvujaji. Badilisha
kama itahitajika.
4.
Badilisha kichujio cha mafuta (A, Kielelezo 14) kwa kichujio halisi cha kubadilisha
sehemu.
5.
Linda njia za mfuta (D, Kielelezo 14) kwa vibanio (C) kama inavyoonyeshwa.
Shughulikia Mfumo wa Kupoesha
Onyo
Injini inayoendesha inazalisha joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa
moto zaidi.
Kuchomeka vikali kunaweza kusababishwa unapogusana nazo.
Uchafu unaoweza kuwaka, kama vile majani, nyasi, brashi, n.k., unaweza
kushika moto.
• Ruhusu mafla, silinda na mapezi ya injini kupoa kabla ya kugusa.
• Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
Notisi
Usitumie maji kusafisha injini. Maji yanaweza kuchafua mfumo wa fueli.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kusafisha injini.
Hii ni injini inayopoeshwa na hewa. Uchafu unaweza kuzuia mtiririko wa hewa na
kusababisha injini kuchemka kupita kiasi, na kusababisha utendakazi mbaya na
kupunguza maisha ya injini.
1.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kuondoa uchafu kutoka kwenye grili ya
kuingiza hewa.
2.
Weka uhusiano, springi na vidhibiti safi.
3.
Weka ene lililo karibu na nyuma ya mafla, iwapo ipo, huru kutokana na uchafu
wowote unaoweza kuwaka.
4.
Hakikisha mapezi ya kupoesha mafuta, iwapo yapo, yako huru kutokana na
uchafu.
Baada ya kipindi cha muda, uchafu unaweza kukusanyika kwenye mapezi ya
kupoesha silinda na kusababisha injini kuwa moto kushinda kiasi. Uchafu huu hauwezi
kuondolewa bila kutokusanyika kwa kiasi fulani kwa injini. Ruhusu Mtoa Huduma wa
Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa kukagua na kusafisha mfumo wa kupoesha hewa
kama ilivyopendekezwa kwenye Ratiba ya Udumishaji.
Hifadhi
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya kuchomeka au kifo.
Wakati wa Kuhifadhi Mafuta Au Kifaa Kilicho na Mafuta Kwenye Tangi
• Hifadhi mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji, au vitu vingine ambavyo
vina taa za moto au vyanzo vya mwako kwa sababu vinaweza kuwasha moto
kwenye mvuke wa mafuta.
Mfumo wa Mafuta
Tazama Kielelezo: 15
Hifadhi kiwango cha injini (mkao wa kawaida wa kuendesha). Jaza tangi la mafuta (A,
Kilelezo 15) kwa mafuta. Ili kuruhusu uvukizi wa mafuta, usijaze kupita chini ya shingo
ya tangi la mafuta (B).
Mafuta yanaweza kuharibika yanapohifadhiwa katika kontena ya uhifadhi kwa zaidi ya
siku 30. Kila mara unapojaza kontena kwa mafuta, ongeza kiimarishaji mafuta kwenye
mafuta kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtengenezaji. Hii inafanya mafuta kukaa
yakiwa safi na kupunguza matatizo yanayohusiana na mafuta au uchafu katika mfumo
wa mafuta.
Si lazima umwage mafuta kutka kwenye injini wakati kiimarishaji mafuta kinapoongezwa
kama ilivyoagizwa. Kabla ya kuendesha, WASHA injini kwa dakika 2 ili kueneza mafuta
na kiimarishaji kote kwenye mfumo wa mafuta.
Ikiwa petroli ndani ya injini haijatibiwa kwa kiimarishaji mafuta, ni lazima imwagwe
kwenye kontena iliyoidhinishwa. Endesha injini hadi isimame kutokana na ukosefu wa
mafuta. Matumizi ya kiimarishaji mafuta kwenye kontena ya uhifadhi yanapendekezwa ili
kudumisha usafi.
Mafuta ya Injini
Wakati injini bado ina joto, badilisha mafuta ya injini. Tazama sehemu Kubadilisha
Mafuta ya Injini.
Utafutatuzi
Kwa usaidizi, wasiliana na mhudumu wa karibu au nenda kwenye
BRIGGSandSTRATTON.com au piga 1-800-233-3723 (Marekani).
Vipimo
Modeli: 400000
Umbali
Kuzalisha
Mpigo
Kiwango cha Mafuta
Nafasi ya Kuziba Cheche
Toku ya Kuziba Cheche
Nafasi ya Koili inayozunguka ya Hewa
Uingizaji wa Vali ya Kuingiza hewa
Uondoaji wa Vali ya Eneo la Kutolea
moshi
Modeli: 440000
Umbali
Kuzalisha
Mpigo
Kiwango cha Mafuta
Nafasi ya Kuziba Cheche
Toku ya Kuziba Cheche
Nafasi ya Koili inayozunguka ya Hewa
Uingizaji wa Vali ya Kuingiza hewa
Uondoaji wa Vali ya Eneo la Kutolea
moshi
40.03 ci (656 cc)
2.970 in (75,43 mm)
2.890 in (73,41 mm)
62 - 64 oz (1,8 - 1,9 L)
.030 in (,76 mm)
180 lb-in (20 Nm)
.008 - .012 in (,20 - ,30 mm)
.004 - .006 in (,10 - ,15 mm)
.004 - .006 in (,10 - ,15 mm)
44.18 ci (724 cc)
3.120 in (79,24 mm)
2.890 in (73,41 mm)
62 - 64 oz (1,8 - 1,9 L)
.030 in (,76 mm)
180 lb-in (20 Nm)
.008 - .012 in (,20 - ,30 mm)
.004 - .006 in (,10 - ,15 mm)
.004 - .006 in (,10 - ,15 mm)
47