Briggs & Stratton 400000 Manual Del Operario página 44

Ocultar thumbs Ver también para 400000:
Tabla de contenido
Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 14
• Jaza tangi la fueli nje au katika eneo linaruhusu hewa kuingia vizuri.
• Usijaze tangi la fueli kupita kiasi. Ili kuruhusu upanukaji wa fueli, usijaze kupita
chini ya shingo la tangi la fueli.
• Hifadhi fueli mbali na cheche, miale iliyo wazi, taa za mwongozo, joto na vyanzo
vingine vya uwakaji.
• Angalia tundu, tangi, kifuniko na kurekebisha mara kwa mara kwa nyufa na uvujaji.
Badilisha ikiwezekana.
• Iwapo fueli itamwagika, subiri hadi ivukize kabla ya kuwasha injini.
1.
Safisha kifuniko cha fueli kutokana na uchafu. Ondoa kifuniko cha fueli.
2.
Jaza tangi la fueli kwa fueli (A, Kielelezo 4). Ili kuruhusu upanuzi wa fueli, usijaze
juu ya chini ya shingo la tangi la fueli (B).
3.
Sakinisha upya kifuniko cha fueli.
Washa na Uzime Injini
Tazama Kelelezo: 5
Washa Injini
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka hara sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
Wakati wa Kuwasha Injini
• Hakikisha kuziba cheche, mafla, kifuniko cha fueli na kisafishaji cha hewa (iwapo
vipo) viko sawa na salama.
• Usiwashe injini wakati kuziba cheche kimeondolewa.
• Iwapo injini inamwaga mafuta, weka choki(iwapo ipo) kwenye eneo la FUNGUA/
ENDESHA, sogeza transfoma ndogo (iwapo ipo) kwenye eneo la HARAKA na
uwashe injini hadi ianze kuenda.
Onyo
MADHARA YA GESI YENYE SUMU. Eneo la injini la kutolea moshi lina
monoksidi kaboni, gesi yenye sumu ambayo inaweza kuua kwa dakika. HUWEZI
kuiona, kuinusa au kuionja. Hata kama huwezi kunusa mafusho yanayotolewa,
unaweza kufikia gesi ya monoksidi kaboni. Iwapo utaanza kuhisi, mgonjwa,
kizunguzungu, au mchovu wakati unatumia bidhaa hii, izime na uende eneo
lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone Daktari. Unaweza kuwa na sumu ya
monoksidi kaboni.
• Endesha bidhaa hii nje TU mbali na madirisha, milango na tundu za kuingiza hewa
ili kupunguza hatari za gesi ya monoksidi kaboni kutokana na kukusanyika na
kuweza kuelekea katika maeneo yaliyo na watu.
• Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa monoksidi kaboni vinavyoendeshwa
na betri pamoja na chelezo za betri kulingana na maelekezo ya mtengenezaji.
Ving'ora vya moshi haviwezi kutambua gesi ya monoksidi kaboni.
• USIENDESHE bidhaa hii nyumbani, karakarani, sehemu ya chini ya majengo,
maeneo ya kutembelea kwenye majengo, vivulini, au maeneo mengine
yaliyofunikwa nusu hata kama unatumia feni au milango na madirisha
yaliyofunguka kuruhusu hewa kuingia. Monoksidi kaboni inaweza kukusanyika
kwa haraka katika maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa, hata baada ya
bidhaa hii kuzimwa.
• KILA MARA weka bidhaa hii katika eneo lenye upepo na uelekeze eneo la kutolea
moshi la injini mbali na maeneo yaliyo na watu.
Notisi
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila mafuta. Kabla uweze kuwasha
injini, hakikisha umeongeza mafuta kulingana na maelekezo kwenye mwongozo
huu. Iwapo utawasha injini bila mafuta, itaharibika hadi kushindwa kukarabatiwa na
hutafidiwa chini ya udhamini huu.
Tambua Mfumo wa Kuwasha
Kabla ya kuwasha injini, lazima utambue aina ya mfumo wa kuanza ambao uko kwenye
injini yako. Injini yako ina mojawapo ya aina zifuatazo.
• Mfumo wa ReadyStart
®
: Hii ina choki otomatiki inayodhibitiwa na halijoto. Haina
prima.
• Mfumo wa Elektroniki wa Kudhibiti Fueli: Hii ina Kitengo cha Kudhibiti cha
Elektroniki kinachofuatilia hali za injini na halijoto. Haina choki kikuli au prima.
• Mfumo wa Choki: Hii ina prima nyekundu inayotumiwa kuwasha katika halijoto
baridi. Baadhi ya modeli zitakuwa na kidhibiti cha choki tofauti na nyingine
zitakuwa na kidhibiti cha choki / transfoma ndogo za pamoja. Aina hizi hazina
prima.
Ili kuwasha injini yako, fuata maelekezo ya aina yako ya mfumo wa kuwasha.
Kumbuka: Kifaa kinaweza kuwa na vidhibiti mbali. Tazama mwongozo wa kifaa kwa
utambuzi na uendeshaji wa vidhibiti mbali.
44
®
Mfumo wa ReadyStart
1.
Angalia mafuta ya injini. Tazama sehemu Kuangalia Kiwango cha Mafuta.
2.
Hakikisha vidhibiti vya kiendeshaji cha kifaa, iwapo vipo, vimetenganishwa.
3.
Sogeza kizima mafuta (A, Kielelezo 5), iwapo kipo, kwenye eneo la FUNGUA.
4.
Sogeza kidhibiti cha transfoma ndogo (B, Kielelezo 5), iwapo kipo, kwenye
sehemu ya HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
Kumbuka: Kwa kuwasha katika halijoto yenye baridi (chini ya nyuzi 32° F), sogeza
mchanganyiko wa choki na wenzo wa transfoma ndogo (B C, Kielelezo 5) kwenye eneo
la IMEFUNGWA.
5.
Geuza swichi ya kianzishi cha umeme (D, Kielelezo 5) kwenye eneo la WASHA au
ANZA au kitufe cha sukuma (E).
Notisi
Ili kurefusha maisha ya kianzishi, tumia misururu mifupi ya kuanzisha
(kiwango cha juu cha sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya mizunguko
inayoanza.
Kumbuka: Iwapo injini haitaanza baada ya majaribio ya kurudia, wasiliana na mtoa
huduma wako wa ndani au nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.com au piga simu
1-800-233-3723 (Marekani).
Mfumo wa Elektroniki wa Kudhibiti Fueli
1.
Angalia mafuta ya injini. Tazama sehemu Kuangalia Kiwango cha Mafuta.
2.
Hakikisha vidhibiti vya kiendeshaji cha kifaa, iwapo vipo, vimetenganishwa.
3.
Sogeza kizima mafuta (A, Kielelezo 5), iwapo kipo, kwenye eneo la FUNGUA.
4.
Sogeza kidhibiti cha transfoma ndogo (B, Kielelezo 5), iwapo kipo, kwenye
sehemu ya HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
5.
Geuza swichi ya kianzishi cha kielektroniki (D, Kielelezo 5) katika sehemu ya
WASHA au ANZA.
Notisi
Ili kurefusha maisha ya kianzishi, tumia misururu mifupi ya kuanzisha
(kiwango cha juu cha sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya mizunguko
inayoanza.
Kumbuka: Iwapo injini haitaanza baada ya majaribio ya kurudia, wasiliana na mtoa
huduma wako wa ndani au nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.com au piga simu
1-800-233-3723 (Marekani).
Mfumo wa Choki

Sogeza kidhibiti cha choki (C, Kielelezo 5), au mchanganyiko wa transfoma ndogo
ya gari na wenzo wa choki (B C, Kielelezo 5), kwenye sehemu ya IMEFUNGWA.
Kumbuka: Kwa kawaida choki haihitajiki wakati wa kuwasha injini iliyochemka.
6.
Geuza swichi ya kianzishi cha kielektroniki (D, Kielelezo 5) katika sehemu ya
WASHA au ANZA.
Notisi
Ili kurefusha maisha ya kianzishi, tumia misururu mifupi ya kuanzisha
(kiwango cha juu cha sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya mizunguko
inayoanza.
7.
Wakati injini inapochemka, sogeza kidhibiti cha choki (C, Kielelezo 5) kwenye
eneo la FUNGUA.
Kumbuka: Iwapo injini haitaanza baada ya majaribio ya kurudia, wasiliana na mtoa
huduma wako wa ndani au nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.com au piga simu
1-800-233-3723 (Marekani).
Simamisha Injini
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka hara sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
• Usiruhusu hewa kuingia kwenye kabureta ili kusimamisha injini.
1.
Sogeza kidhibiti cha transfoma ndogo (B, Kielelezo 5) katika eneo la POLEPOLE.
2.
Geuza ufunguo wa swichi (D, Kielelezo 5) kwenye eneo la ZIMA. Ondoa ufunguo
na uhifadhi katika sehemu salama kutokana na ufikiaji wa watoto.
BRIGGSandSTRATTON.com
Tabla de contenido
loading

Este manual también es adecuado para:

440000490000

Tabla de contenido