Briggs & Stratton 080000 Manual Del Operador página 45

Ocultar thumbs Ver también para 080000:
Tabla de contenido
Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 14
Notisi
Ili kurefusha muda wa kianzishaji, tumia misururu mifupi ya kuanzisha (upeo
wa sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya mizunguko inayoanza.
10.
Injini inapochemka, songeza kidhibiti cha choki (F, Kielelezo 11) hadi eneo la
kuonyesha IMEFUNGULIWA / ENDESHA (OPEN / RUN).
Kumbuka: Injini ikikosa kuwasha baada ya majaribio kadhaa, wasiliana na mtoa huduma
wako wa ndani au nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.com au upige simu kwa
1-800-233-3723 (nchini Marekani).
Mfumo wa Prima
1.
Kagua oili ya injini. Tazama sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili .
2.
Hakikisha vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo, vimezimwa.
3.
Bonyeza swichi ya kusimamisha (A, Kielelezo 12), ikiwa ipo, hadi eneo la
kuonyesha IMEWASHWA.
4.
Songeza kidhibiti Injini (B, Kielelezo 12), ikiwa kipo, kwenye nafasi ya HARAKA.
Endesha injini ikiwa katika nafsi HARAKA.
5.
Sukuma prima nyekundu (F, Kielelezo 12) mara tatu (3).
Kumbuka: Kila mara uaandaji hauhitajiki wakati wa kuanzisha tena injini iliyo chemka.
Kumbuka: Iwapo utasukuma prima mara nyingi zaidi, fueli ya kupita kiasi itamwagika
kwenye injini na itakuwa vigumu kuwasha.
6.
Ondosha wenzo wa kusimamisha injini (C, Kielelezo 10), ikiwa upo, dhidi ya kipini.
7.
Kwa uthabiti shikilia kamba ya kishikilio cha kianzishi (D, Kielelezo 12). Vuta
kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi inakuwa gumu kuvuta, kisha uvute kwa
haraka.
Onyo
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishi (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia. Mifupa
ilivyovunjika, kuvunjika kwa mifupa mikuuu, michubuko, mishtuko inaweza kutokea.
Wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi inakuwa
gumu kuvuta na kisha uvute kwa haraka ili kuzuia kuvutwa nyuma kwa haraka.
Kumbuka: Iwapo injini haitaanza baada ya majaribio kadhaa, rudia Hatua 5,6, na 7.
Iwapo bado haianzi, wasiliana na mtoa huduma wako wa ndani au nenda kwenye
BRIGGSandSTRATTON.com au upige simu kwa 1-800-233-3723 (nchini Marekani).
Simamisha Injini
Onyo
Mafuta pamoja na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo.
• Usikabe, iwapo kipo, kabiureta ili kusimamisha injini.
1.
Wenzo wa Kusimamisha Ijini, iwapo upo: Ondosha wenzo wa kusimamisha
injini (E, Kielelezo 10).
Swichi ya Kusimamisha, iwapo ipo: Songeza swichi ya kusimamisha (D,
Kielelezo 9, 11, A, Kielelezo 12) hadi kwenye eneo la kuonyesha ZIMA .
Kidhibiti Injini, iwapo kipo: Songeza kidhibiti Injini (B, Kielelezo 8, 12) kwenye
eneo la kuonyesha SIMAMISHA.
Ufunguo wa Kianzishaji kwa Umeme, iwapo upo: Geuza ufunguo wa
kianzishaji hadi eneo la ZIMA / SIMAMISHA (OFF / STOP). Ondoa ufunguo na
uuweke katika mahali salama mbali na watoto.
2.
Baada ya injini kusimamishwa, songeza vali ya kufungia mafuta (A, Kielelezo 8),
ikiwa ipo, hadi kwenye eneo la kuonyesha IMEFUNGWA (CLOSED).
Udumishaji
Notisi
Iwapo injini imeinamishwa wakati wa udumishaji, tangi la fueli, iwapo liko
kwenye injini, lazima liwe tupu na upande wa kuziba cheche lazima uwe juu. Iwapo
tangi la fueli sio tupu na iwapo injini imeinamishwa katika mwelekeo mwingine,
inaweza kuwa vigumu kuwaka kwa sababu ya mafuta au petroli kuchafua kuchuja
hewa na/au kuziba cheche.
Onyo
Wakati unapotekeleza udumishaji unaohitaji kitengo kuinamishwa, tangi la fueli,
iwapo limewekwa kwenye injini, lazima liwe tupu au fueli inaweza kumwagika nje na
kusababisha moto au mlipuko.
Tunapendekeza kuwa umwone Mtoa Huduma yeyote wa Briggs & Stratton
Aliyeidhinishwa kwa udumishaji na huduma zote za injini na sehemu za injini.
Notisi
Vijenzi vyote vilivyotumiwa kujenga injini hii lazima visalie sawa kwa
uendeshaji bora.
Onyo
Cheche zisizotarajiwa zinaweza kusababisha moto au mshtuko wa kielektriki.
Uwashaji usiotarajiwa unaweza kusababisha kunaswa, kukatwa kwa viungo
kwa kiwewe, au majeraha makali ya ukataji wa ngozi.
Madhara ya moto
Kabla ya kutekeleza marekebisho au ukarabati:
• Tenganisha waya ya kuziba cheche na uhifadhi mbali na kuziba cheche.
• Tenganisha betri katika mwisho wa chanya (injini zilizo na kiwashaji wa kielektriki
tu.)
• Tumia zana sahihi tu.
• Usihitilifiane na springi ya kithibiti, viunganishi au sehemu zingine ili kuongeza kasi
ya injini.
• Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa katika eneo sawa
kama sehemu asili. Sehemu zingine huenda zisitekeleze vilevile, zinaweza
kuharibu kitengo, na inaweza kusababisha majeraha.
• Usigonge gurudumu la kuongeza kasi ya injini kwa nyundo au kifaa kigumu
kwa sababu gurudumu la kuongeza kasi ya injini linaweza kuvunjika wakati wa
kuendesha.
Wakati wa kujaribu cheche:
• Tumia kijaribio cha kuziba cheche kilichoidhinishwa.
• Usikague injini wakati kuziba cheche imeondolewa.
Huduma ya Udhibiti wa Mafukizo
Udumishaji, ubadilishaji, au ukarabati wa vifaa na mifumo ya kudhibiti mafukizo
unaweza kutekelezwa na kituo chochote au mtu yeyote wa kukarabati injini. Hata
hivyo, ili kupata huduma ya kudhibiti mafukizo ya "bila malipo", ni lazima kazi ifanywe na
mtoa huduma aliyeidhinishwa na kiwanda. Tazama Taarifa ya Udhibiti wa Mafukizo.
Ratiba ya Udumishaji
Saa 5 za Kwanza
• Badilisha oili ( Hakuhitajiki kwenye miundo ya Just Check & Add™ )
Kila Baada ya Saa 8 au Kila Siku
• Kagua kiwango cha oili ya injini
• Safisha eneo karibu na mafla na vidhibiti
• Safisha grili ya kuingiza hewa
Kila Baada ya Saa 25 au Kila mwaka
• Safisha chujio la hewa
1
• Safisha kisafishaji cha mwanzo (iwapo kipo)
Kila Baada ya Saa 50 au Kila mwaka
• Badilisha oili ya injini (Hakuhitajiki kwenye Just Check & Add™ )
• Fanyia huduma mfumo wa ekzosi
Kila Mwaka
• Badilisha plagi ya spaki
• Badilisha chujio la hewa
• Badilisha kisafishaji cha mwanzo (iwapo kipo)
• Fanyia huduma mfumo wa kupoesha
• Kagua uwazi wa vali
2
1
Katika hali za vumbi au wakati uchafu unaosambazwa na hewa upo, safisha
mara kwa mara.
2
Haihitajiki isipokuwa matatizo ya utendakazi wa injini yatambuliwa.
Kabureta na Kasi ya Injini
Kamwe usifanye marekebisho kwenye kabureta au kasi ya injini. Kabureta iliwekwa
kwenye kiwanda kufanya kazi kwa ufanisi chini ya masharti mengi. Usihitilafiane na
springi ya kidhibiti, uhusiano au sehemu nyingine ili kubadilisha kasi ya injini. Iwapo
marekebisho yoyote yanahitajika wasiliana na Mtoa Huduma wa Briggs & Stratton
Aliyeidhinishwa kwa huduma.
1
45
Tabla de contenido
loading

Este manual también es adecuado para:

090000093j00100000

Tabla de contenido